Monday, April 13, 2015

NDIYO MALIMWENGU BIBI WA UMRI WA MIKA 65,ANA MIMBA YA PACHA WANNE
Bi Annegret Raunigk
Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Berlin Ujerumani ambaye ana watoto kumi na watatu ametangaza kuwa ni mja mzito na pacha wanne.
Kwa mwaka mmoja unusu sasa , bi Annegret Raunigk ambaye ni mwalimu wa kingereza na kirusi amekuwa akijaribu kupata mtoto mwingine kwa njia ya upandikizaji, Kulingana na vyombo vya habari vya German RTL.
Bibi huyo anasema kuwa alilazimika kuwatafuta watoto zaidi baada ya kitinda mimba wake mwenye umri wa miaka 9 kumsihi umtafutia watoto atakaocheza nao.
Bi Raunigk, ambaye amebeba mimba hiyo kwa majuma 21 sasa anasema kuwa alishtuka kujua kuwa alikuwa amejaaliwa mimba ya watoto 4 wala sio mmoja kama alivyotarajiwa.
Bi Raunigk aliyechangiwa mayai na mbegu za kiume anawatoto wengine 13 kutoka kwa baba watano tofauti.
Aidha mwanawe Leila alizua majadala mkali alipozaliwa mwaka wa 2005 lakini hilo halimsumbui bibi huyo ambaye miaka kumi ijayo atakuwa na tineja na watoto wachanga.
Mwanawe wa kwanza ana miaka 44.
Mahojiano ya bibi huyo na runinga hiyo ya kijerumani yanatarajiwa kuvutia hisia nyingi itakapopeperushwa baadaye leo.
Mbali na kufurahiwa wanawe 13 Bi Raunigk anawajukuu 7.
Kufikia sasa mimba hii ya kihistoria haijaonesha hitilafu yeyote.
Kufikia sasa mwanamke anayeshikilia rekodi duniniani ya kuwa mama aliyejifungua pacha wanne ni Merryl Fudel,aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 55.
Vilevile mwanamke ambaye anashikilia rekodi ya kujifungua akiwa na umri mkubwa zaidi ni Omkari Panwar, kutoka India aliyejifungua akiwa na miaka 70.

Thursday, February 19, 2015

BWANA HARUSI AANGUKA KIFAFA KABLA YA HARUSI, ALIMFICHA MKEWE MTARAJIWA KAMA ANAANGUKA, MKE AAMUA KUOLEWA NA MWINGINE  PAPO KWA PAPO

Bi harusi mmoja kaskazini mwa nchi ya India alifanya maamuzi ya papo kwa hapo kuolewa na mmoja wa wageni waliofika kushereheka naye katika harusi yake baada ya mumewe kuugua ghafla.
Mwanamke huyo ajulikanaye kama Indra anayetokea Rampur jimbo la Uttar Pradesh, inaelezwa kuwa sekunde chache kabla ya ndoa ya wawili hao mume akaanguka kifafa, na hivyo kumlazimu kuondoka harusini na kwenda kumwona daktari.
Bi harusi Indra, alishikwa na hasira ya hali ya juu, kwakuwa mume alimficha juu ya hali yake, naye hakuwahi kujua hata siku moja kuwa , jamaa ana tatizo la kuanguka kifafa.
Indra akatoa ombi lake kuwa anahitaji kuolewa na mmoja wa wana familia ya bwana harusi , ambaye alikuja harusini kusherehekea harusi ya nduguye,na Indra akamtaka achukue nafasi ya nduguye badala yake, jamaa akaona nyota ya jaha imemuangukia, si akakubali !
Ndoa ikafungwa, hali ya bwana harusi wa kwanza mwenye kuanguka kifafa, haijajulikana mpaka harusi ya pili ilipokwisha.

Monday, February 9, 2015

Mwali huyo
Kipa wa Ivory Coast Boubacar Barry akifunga penati ya mwisho ya ushindi
Shamla shamla za ushindi
Kocha wa Ivory Coast Herve Renard akiongoza ushangiliaji


Ivory Coast wameibuka Bingwa wa Mataifa ya Afrika kwenye Mechi ya Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, walipoibwaga Ghana kwa Mikwaju ya Penati 9-8 Jana Usiku huko Estadio de Bata, Mjini Bata Nchini Equatorial Guinea, kama walivyofanya Mwaka 1992.
Hii ni mara ya pili kwa Ivory Coast kutwaa Ubingwa wa Afrika na mara ya kwanza ni Mwaka 1992 walipoitoa Ghana pia kwa Mikwaju ya Penati 11-10 baada ya suluhu ya 0-0.
Hii pia ni mara ya pili kwa Kocha wa Ivory Coast, Herve Renard, kutwaa Ubingwa wa Afrika na mara ya kwanza ilikuwa 2012 alipoiwezesha Zambia kutwaa Ubingwa, tena kwa kuifunga Ivory Coast, na sasa kuweka Rekodi ya kuwa Mtu wa kwanza kutwaa Ubingwa wa Afrika na Nchi mbili tofauti.
Hapo Jana Shujaa wa Ivory Coast ni Kipa wao Boubacar Barry ambae aliokoa na pia kufunga Penati muhimu iliyowapa Ivory Coast Ubingwa.
Kila Timu ilikosa Penati 5 na ndipo Kipa Barry akaokoa Penati iliyopigwa na Kipa mwenzake Brimah Razak na kisha kufunga Penati ya ushindi.
Kwa Kocha wa Ghana, Avram Grant, hii ni mara ya pili kushindwa Fainali kubwa kwa Mikwaju ya Penati baada ya Mwaka 2008, akiwa na Chelsea, alipobwagwa kwa Mikwaju ya Penati na Manchester United kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Moscow, Urusi.
Ghana, ambao mara ya mwisho kati ya mara zao 4 kuwa Bingwa wa Afrika ilikuwa 1982, wangeweza kushinda Fainali hii hasa baada ya kupata nafasi kadhaa katika Dakika 120 za Mchezo na mara mbili kupiga Posti.
Pia hata kwenye Mikwaju ya Penati walianza kwa mguu mzuri pale Ivory Coast walipokosa Penati zao 2 za kwanza kwa Mchezaji mpya wa Manchester City, Wilfried Bony, kupiga Posti na Junior Tallo kutoa nje lakini Ghana nao, kupitia Afriyie Acquah na Frank Acheampong, wakakosa.
Baada ya Wachezaji wote wa ndani kumaliza kupiga Penati zao ikaja zamu za Makipa na ndipo Kipa Boubacar Barry akaokoa Penati iliyopigwa na Kipa mwenzake Brimah Razak na kisha kufunga Penati ya ushindi kwa Ivory Coast kutwaa Ubingwa kwa Penati 9-8.
VIKOSI:
Ivory Coast: Barry, Kolo Toure, Tiene (Kalou - 116'), Gervinho (Gadji-Celi Carmel Junior - 122'), Bony, Gradel (Doumbia - 67'), Aurier, Yaya Toure, Gonzaroua Die, Bailly, Kanon.
GhanaBrimah, Afful, Rahman, Mensah, Boye, Wakaso, Acquah, Ayew, Atsu (Acheampong - 116'), Gyan (Badu - 121'), Appiah J.Ayew - 99').
2015 AFCON Matokeo ya awali:
Ivory Coast:
1-1 na Guinea
1-1 na Mali
1-0 ushindi na Cameroon
3-1 ushindi na Algeria
3-1 ushindi na DR Congo

Ghana:
1-2 kipigo na Senegal
1-0 ushindi na Algeria
2-1 ushindi na South Africa
3-0 ushindi na Guinea
3-0 ushindi na Equatorial Guinea

MSHINDI WA 3
Jumamosi Februari 7
Congo DR 0 Equatorial Guinea 0 [Penati 4-2]  
FAINALI
Jumapili Februari 8
Ivory Coast 0 Ghana 0 [Penati 9-8]     
Listi ya FIFA Ubora Duniani:
Ivory Coast: Nafasi ya 28
Ghana: Nafasi ya 37

Friday, February 6, 2015

AFCON 2015: GHANA WATINGA FAINALI KUWAVAA IVORY COAST JUMAPILI, MALABO WAGEUKA UWANJA WA VITA


WANA wa Nguli wa Soka Afrika, Abedi Ayew Pele, wameiongoza Nchi yao Ghana kuwateketeza Wenyeji Equatorial Guinea kwa kuichapa Bao 3-0 katika Mechi ya Nusu Fainali ya Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, iliyochezwa Nuevo Estadio de Malabo, Mjini Malabo.

Watoto hao wa Abedi Pele, Andre Ayew na Jordan Ayew, kila mmoja alipiga Bao moja na Wakaso kufunga jingine kwenye Mechi ambayo Ghana waliongoza 2-0 hadi Mapumziko lakini walishindwa kuingia Vyumba vya Kubadili Jezi wakati huo baada ya Mashabiki wa Wenyeji Equatorial Guinea kupandwa jazba na kuirushia Timu ya Ghana vitu na kulazimu Polisi kuingilia kati.
Huku Washabiki hao wakitangaziwa kuwa Mechi hiyo itavunjwa na ulinzi kuimarishwa Kipindi cha Pili kilichezwa na Ghana kupiga Bao lao la Tatu.
Bao za Ghana zilifungwa na Penati ya Jordan Ayew Dakika ya 42, Wakaso Dakika ya 45, na Andre Ayew Dakika ya 75.
Gemu hii ilisimama Dakika ya 84 baada ya Washabiki wa Ghana kukimbilia Uwanjani toka Jukwaani wakihofia usalama wao baada ya kushambuliwa na Mashabiki wa Equatorial Guinea. Baada ya Nusu Saa, kwa msaada wa Helikopta na Polisi, Mechi ilianza tena na kuchezwa Dakika zilizosalia huku Uwanja ukiwa mtupu baada ya Watazamaji wengi kuondoka.
Ghana, ambao washawahi kuwa Mabingwa wa Afrika mara 4 ingawa hawajatwaa Ubingwa huo tangu 1982, wanatinga Fainali kucheza na Ivory Coast ambayo haijawahi kuwa Bingwa ingawa safari hii imesheheni Mastaa kibao wanaocheza Ulaya.
Jumatano Usiku, kwenye Nusu Fainali ya kwanza, Ivory Coast iliichapa Congo DR Bao 3-1.
Fainali itachezwa Jumapili ndani ya Estadio de Bata, Mjini Bata.

Thursday, January 29, 2015

DUNIANI KUNA VITUKO, 'AJIOA' BAADA YA KUKOSA MCHUMBA
Mwanamke mmoja nchini Marekani Yasmin Eleby hakupata mchumba wa kumuoa  ambaye alitaka awe mume wake atakapofikisha miaka 40, ameamua kufanya kitendo ambacho kimewashangaza wengi, kwa kujioa mwenyewe.
Kwa mujibu wa mtandao wa MySanAntonio.com,Eleby aliahidi kwamba ikiwa hatapata mchumba wakati atakapokuwa ametimiza miaka 40, basi atafanya harusi ya mtu mmoja yaani atajioa ili kusherehekea miaka yake 40.
Duru zinasema kuwa mwanamke Eleby alifanya harusi yake mwenyewe katika makavazi ya Houston akiambatana na jamaa na familia yake na wageni wengine waalikwa.
Kwa sherehe hii, dadake Eleby ndiye aliendesha sherehe hio, kwani ni kinyume na sheria kwa mtu kujioa mwenyewe. Harusi ya kawaida ni kati ya watu wawili.
Katika picha za kanisani sherehe ilionekana kuwa ya kawaida bila ya mchumba.
Kulingana na John Guess Jr afisaa mkuu wa makavazi hayo, sherehe hiyo ilionekana kuwa bila tashwishi na kuonekana kama jambo la kawaida kwani makavazi hayo huwakumbatia watu wa jinsia mbali mbali kuendesha harusi zao hapo.
Aliposikia kwamba Eleby, ambaye anaishi na kufanya kazi ugenini alikuwa anapanga kujioa mwenyewe, aliharakisha kwenda katika eneo hilo kujionea mwenyewe.
"Eleby alipofikisha umri wa miaka 40 bila ya kupata mpenzi na mtu mwenye nia ya kumuoa, aliamua angejioa mwenyewe,''alisema Guess Jr ambaye anasema harusi hiyo imewashangaza wengi na kuwa gumzo katika mitandao ya kijamii.
Anasema anakubaliana na Eleby na mtazamo wake wa mapenzi kwamba mtu anaweza kujipenda na kujioa kwa kukosa wa kumuoa kwani cha muhimu ni mtu kujipenda kwanza kabla ya kupendwa.
"watu wengu huolewa bila ya kutafakari mara mbili kuhusu yule anayemuoa, '' Guess Jr alisema.
Anadhani kwamba pindi watu watakapomuona Eleby anavyojishughulikia mwenyewe, huenda akapata ushindani.
"ni mrembo, anafanya kazi kwa bidii na anasifika duniani na pia anaona uamuzi wake umewapa gumzo watu wengi. ''
KUNDI D la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, limemaliza Mechi zao za mwisho kwa Ivory Coast kutinga Robo Fainali baada ya kuifunga Cameroun lakini Mali na Guinea zinangoja kurushwa Shilingi kuamua nani ataungana nao baada ya Timu hizo kutoka Sare kwenye Mechi yao ya mwisho na kufungana kwa kila kitu.
Ivory Coast wametinga Robo Fainali baada ya kuifunga Cameroun Bao 1-0 na kutwaa uongozi wa Kundi D katika dimba la  Nuevo Estadio de Malabo, Mjini Malabo.
Ivory Coast walitinga Haftaimu wakiwa Bao 1-0 mbele kwa Bao la Dakika ya 36 la Max-Alain Gradel kwa Shuti la Mita 30.
Na katika dimba la Estadio de Mongomo, Mjini Mongomo, Guinea walitangulia kupata Bao lao kwa Penati iliyotolewa Dakika ya 13 kufuatia Wague kuunawa Mpira na Kevin Constant kufunga Penati hiyo.
Mali walishindwa kusawazisha Dakika chache baadae baada ya wao pia kupewa Penati kufuatia Issiaga Sylla kuunawa lakini Seydou Keita alipiga Penati dhaifu iliyookolewa na Kipa Naby Yattara, Hadi Mapumziko Guinea 1 Mali 0.
Kipindi cha Pili Modibo Maiga, Mchezaji wa West Ham anacheza kwa Mkopo Metz ya France, aliawazisha kwa Mali kwa Kichwa baada ya Krosi ya Abdoulay Diaby.
Timu zote mbili Guinea na Mali zote zina pointi sawa na magoli matatu ya kufunga.
Kwa sasa timu moja kati ya Guinea au Mali itasonga mbele hatua ya robo fainali baada ya kura itakayopigwa hii leo na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF.

Tuesday, January 27, 2015

                 
KUNDI B la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, limecheza Mechi zao za mwisho ambazo zote mbili ziliisha kwa Sare ambazo zimewanufaisha Tunisia na Congo DR kutinga Robo Fainali huku Cape Verde na Zambia wakitupwa nje.

Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekuwa timu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kusonga  hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ya Afrika baada ya kutoka sare ya goli moja kwa moja na Tunisia.
Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesonga mbele baada ya kumaliza ikiwa ya pili kwenye kundi B nyuma ya Tunisia ambayo nayo pia imesonga mbele ikiwa ndio inayoongoza kundi hilo.
Pamoja na kwamba imemaliza ikiwa na pointi sawa na Cape Verde idadi kubwa ya magoli iliyofunga ndio iliyowavukisha.
Goli la pekee la Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambalo ndilo lililowavukisha kusonga mbele lilifungwa na Jeremy Bokila. Na lile la Tunisia lilifungwa na Ahmed Akaichi.
Kwa upande mwingine timu nyingine kutoka ukanda wa Afrika Mashariki na kati timu ya taifa ya Zambia Chipolopolo imefungasha virago kwenye mashindano hayo baada ya kumaliza ikiwa ya mwisho kwenye kundi hilo baada ya kutoka sare ya kutokufungana na Cape Verde.
Zambia ambaye ni Bingwa wa Kombe hilo mwaka 2012 na Cape Verde zote zimeyaaga mashindano hayo.
Zambia ilihitaji kushinda mechi hiyo japo kwa goli moja lakini bahati haikuwa yao kwani mwamwizi wa mpambano huo Néant Alioum alipopuliza kipenga cha mwisho matokeo yakabaki Zambia 0 Cape Verde 0.
Kwa matokeo hayo sasa Timu ya DRC itakutana na majirani zao  Congo Brazaville katika hatua ya robo fainali huku Tunisia wao wakikutana na wenyeji Equatorial Guinea
Wakati mashabiki wa huko Lusaka na maeneo mengine nchi Zambia wakiwa majozi kwa upande wao mashabiki wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambao timu yao imesonga mbele wamekesha kwa furaha usiku kucha.

Monday, January 26, 2015

MSIMAMO WA LIGI KUU BAADA YA MECHI ZA JUZI NA JANA

Jumamosi Januari 24
Polisi Morogoro 0 Yanga 1

Jumapili Januari 25
Azam FC 1 Simba 1
Stand United 0 Coastal Union 1
Mbeya City 2 Tanzania Prisons 2
Ruvu Shooting 2 Mtibwa Sugar 1
JKT Ruvu 1 Mgambo JKT 1
Kagera Sugar 1 Ndanda FC 2 [CCM Kirumba, Mwanza]

MSIMAMO
NA
TIMU
P
W
D
L
F
 A

GD
PTS
1
Azam FC
11
6
3
2
15
8

7
21
2
Yanga
10
5
3
2
12
7

5
18
3
JKT Ruvu
12
5
3
4
12
11

1
18
4
Mtibwa Sugar
10
4
5
1
13
7

6
17
5
Coastal Union
11
4
4
3
10
8

2
16
6
Polisi Moro
12
3
6
3
9
9

0
15
7
Ruvu Shooting
12
4
3
5
7
9

-2
15
8
Kagera Sugar
12
3
5
4
9
10

-1
14
9
Mgambo JKT
11
4
2
5
6
10

-4
14
10
Simba
10
2
7
1
10
8

2
13
11
Ndanda FC
12
4
1
7
12
17

-5
13
12
Mbeya City
10
3
3
4
6
8

-2
12
13
Stand United
12
2
5
5
7
14

-7
11
14
Tanzania Prisons
11
1
6
4
8
10

-2
9