Mwali huyo |
Kipa wa Ivory Coast Boubacar Barry akifunga penati ya mwisho ya ushindi |
Shamla shamla za ushindi |
Kocha wa Ivory Coast Herve Renard akiongoza ushangiliaji |
Hii ni mara ya pili kwa Ivory Coast kutwaa Ubingwa wa Afrika na mara ya kwanza ni Mwaka 1992 walipoitoa Ghana pia kwa Mikwaju ya Penati 11-10 baada ya suluhu ya 0-0.
Hii pia ni mara ya pili kwa Kocha wa Ivory Coast, Herve Renard, kutwaa Ubingwa wa Afrika na mara ya kwanza ilikuwa 2012 alipoiwezesha Zambia kutwaa Ubingwa, tena kwa kuifunga Ivory Coast, na sasa kuweka Rekodi ya kuwa Mtu wa kwanza kutwaa Ubingwa wa Afrika na Nchi mbili tofauti.
Hapo Jana Shujaa wa Ivory Coast ni Kipa wao Boubacar Barry ambae aliokoa na pia kufunga Penati muhimu iliyowapa Ivory Coast Ubingwa.
Kila Timu ilikosa Penati 5 na ndipo Kipa Barry akaokoa Penati iliyopigwa na Kipa mwenzake Brimah Razak na kisha kufunga Penati ya ushindi.
Kwa Kocha wa Ghana, Avram Grant, hii ni mara ya pili kushindwa Fainali kubwa kwa Mikwaju ya Penati baada ya Mwaka 2008, akiwa na Chelsea, alipobwagwa kwa Mikwaju ya Penati na Manchester United kwenye Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Moscow, Urusi.
Ghana, ambao mara ya mwisho kati ya mara zao 4 kuwa Bingwa wa Afrika ilikuwa 1982, wangeweza kushinda Fainali hii hasa baada ya kupata nafasi kadhaa katika Dakika 120 za Mchezo na mara mbili kupiga Posti.
Pia hata kwenye Mikwaju ya Penati walianza kwa mguu mzuri pale Ivory Coast walipokosa Penati zao 2 za kwanza kwa Mchezaji mpya wa Manchester City, Wilfried Bony, kupiga Posti na Junior Tallo kutoa nje lakini Ghana nao, kupitia Afriyie Acquah na Frank Acheampong, wakakosa.
Baada ya Wachezaji wote wa ndani kumaliza kupiga Penati zao ikaja zamu za Makipa na ndipo Kipa Boubacar Barry akaokoa Penati iliyopigwa na Kipa mwenzake Brimah Razak na kisha kufunga Penati ya ushindi kwa Ivory Coast kutwaa Ubingwa kwa Penati 9-8.
VIKOSI:
Ivory Coast: Barry, Kolo Toure, Tiene (Kalou - 116'), Gervinho (Gadji-Celi Carmel Junior - 122'), Bony, Gradel (Doumbia - 67'), Aurier, Yaya Toure, Gonzaroua Die, Bailly, Kanon.
Ghana: Brimah, Afful, Rahman, Mensah, Boye, Wakaso, Acquah, Ayew, Atsu (Acheampong - 116'), Gyan (Badu - 121'), Appiah J.Ayew - 99').
2015 AFCON Matokeo ya awali:
Ivory Coast:
1-1 na Guinea
1-1 na Mali
1-0 ushindi na Cameroon
3-1 ushindi na Algeria
3-1 ushindi na DR Congo
Ghana:
1-2 kipigo na Senegal
1-0 ushindi na Algeria
2-1 ushindi na South Africa
3-0 ushindi na Guinea
3-0 ushindi na Equatorial Guinea
MSHINDI WA 3
Jumamosi Februari 7
Congo DR 0 Equatorial Guinea 0 [Penati 4-2]
FAINALI
Jumapili Februari 8
Ivory Coast 0 Ghana 0 [Penati 9-8]
Listi ya FIFA Ubora Duniani:
Ivory Coast: Nafasi ya 28
Ghana: Nafasi ya 37
No comments:
Post a Comment