KUNDI D la Mashindano ya Mataifa ya Afrika, AFCON 2015, limemaliza
Mechi zao za mwisho kwa Ivory Coast kutinga Robo Fainali baada ya kuifunga
Cameroun lakini Mali na Guinea zinangoja kurushwa Shilingi kuamua nani
ataungana nao baada ya Timu hizo kutoka Sare kwenye Mechi yao ya mwisho na
kufungana kwa kila kitu.
Ivory Coast wametinga Robo Fainali baada ya kuifunga
Cameroun Bao 1-0 na kutwaa uongozi wa Kundi D katika dimba la Nuevo Estadio de Malabo, Mjini
Malabo.
Ivory Coast walitinga Haftaimu wakiwa Bao 1-0 mbele kwa
Bao la Dakika ya 36 la Max-Alain Gradel kwa Shuti la Mita 30.
Na
katika dimba la Estadio de Mongomo, Mjini Mongomo, Guinea walitangulia kupata Bao lao kwa Penati
iliyotolewa Dakika ya 13 kufuatia Wague kuunawa Mpira na Kevin Constant kufunga
Penati hiyo.
Mali walishindwa kusawazisha Dakika chache baadae baada
ya wao pia kupewa Penati kufuatia Issiaga Sylla kuunawa lakini Seydou Keita
alipiga Penati dhaifu iliyookolewa na Kipa Naby Yattara, Hadi Mapumziko Guinea
1 Mali 0.
Kipindi cha Pili Modibo Maiga, Mchezaji wa West Ham
anacheza kwa Mkopo Metz ya France, aliawazisha kwa Mali kwa Kichwa baada ya
Krosi ya Abdoulay Diaby.
Timu zote
mbili Guinea na Mali zote zina pointi sawa na magoli matatu ya kufunga.
Kwa sasa
timu moja kati ya Guinea au Mali itasonga mbele hatua ya robo fainali baada ya
kura itakayopigwa hii leo na Shirikisho la Soka barani Afrika CAF.
No comments:
Post a Comment