NDIYO MALIMWENGU BIBI WA UMRI WA MIKA 65,ANA MIMBA YA PACHA WANNE
Bi Annegret Raunigk |
Mwanamke
mmoja mwenye umri wa miaka 65 kutoka Berlin Ujerumani ambaye ana watoto kumi na
watatu ametangaza kuwa ni mja mzito na pacha wanne.
Kwa mwaka
mmoja unusu sasa , bi Annegret Raunigk ambaye ni mwalimu wa kingereza na kirusi
amekuwa akijaribu kupata mtoto mwingine kwa njia ya upandikizaji, Kulingana na
vyombo vya habari vya German RTL.Bibi huyo anasema kuwa alilazimika kuwatafuta watoto zaidi baada ya kitinda mimba wake mwenye umri wa miaka 9 kumsihi umtafutia watoto atakaocheza nao.
Bi Raunigk, ambaye amebeba mimba hiyo kwa majuma 21 sasa anasema kuwa alishtuka kujua kuwa alikuwa amejaaliwa mimba ya watoto 4 wala sio mmoja kama alivyotarajiwa.
Bi Raunigk aliyechangiwa mayai na mbegu za kiume anawatoto wengine 13 kutoka kwa baba watano tofauti.
Aidha mwanawe Leila alizua majadala mkali alipozaliwa mwaka wa 2005 lakini hilo halimsumbui bibi huyo ambaye miaka kumi ijayo atakuwa na tineja na watoto wachanga.
Mwanawe wa kwanza ana miaka 44.
Mahojiano ya bibi huyo na runinga hiyo ya kijerumani yanatarajiwa kuvutia hisia nyingi itakapopeperushwa baadaye leo.
Mbali na kufurahiwa wanawe 13 Bi Raunigk anawajukuu 7.
Kufikia sasa mimba hii ya kihistoria haijaonesha hitilafu yeyote.
Kufikia sasa mwanamke anayeshikilia rekodi duniniani ya kuwa mama aliyejifungua pacha wanne ni Merryl Fudel,aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 55.
Vilevile mwanamke ambaye anashikilia rekodi ya kujifungua akiwa na umri mkubwa zaidi ni Omkari Panwar, kutoka India aliyejifungua akiwa na miaka 70.
No comments:
Post a Comment