MAREKANI YARUHUSU MFUNGWA KUOA
Charles Manson |
Mtu
aliyeua watu wengi nchini Marekani na kufungwa kifungo cha maisha Charles
Manson, mwenye umri wa miaka 80, ameripotiwa kupewa hati ya kuoana na mwanamke
mwenye umri wa miaka 26 ambaye amekuwa akimtembelea gerezani.
Hati
hiyo ya ndoa ilitolewa siku 10 zilizopita kwa Manson na Afton Elaine Burton,
limeripoti shirika la habari la Associated Press.
Bi
Burton alihamia Corcoran, California, miaka tisa iliyopita ili kuwa karibu na
gereza la Manson.
Manson
anatumikia kifungo cha maisha jela kwa kuua watu saba na mtoto mmoja ambaye
hakuwa amezaliwa huko Los Angeles Marekani mwaka 1969.
Waliouawa
ni pamoja na mwigizaji aliyekuwa mjamzito Sharon Tate, mke wa mwongoza sinema
Roman Polanski.
Charles
Manson mfungwa mweye umri wa miaka 80 na mke mtarajiwa Afton Elaine
Burton"Star" miaka 26
Bi
Burton, ambaye anajiita nyota, ameliambia shirika la Associated Press kuwa
ataoana na Manson mwezi ujao. Hati hiyo imeripotiwa kudumu kwa siku 90.
"Wote
mtajua kuwa ni kweli... Itatokea," ameliambia shirika hilo.
"Nampenda,"
ameongeza kusema.
Kiongozi
huyo wa kidini na wafuasi wake, wakijulikana kama Familia ya Manson, aliwachoma
visu na kuwaua kwa kuwapiga risasi watu saba huko Los Angeles katika siku mbili
mwezi Agosti 1969 katika jaribio la kutaka kuanza vita vipya vya matabaka ya
rangi.
Manson
na wanawake watatu washirika wake walihukumiwa adhabu ya kifo kutokana na
mauaji hayo, lakini hukumu hiyo ilitolewa mwaka 1972 wakati jimbo la California
lilipositisha kwa muda adhabu ya kifo.
Mwaka
2012, Manson alinyimwa parole yaani msamaha wa kuachiliwa na jopo la gereza la
California - ilikuwa mara ya 12 kwa Manson kuomba kuachiliwa huru.
Kwa
matokeo hayo, Manson hastahili tena kuomba parole hadi mwaka 2027.
BBC
No comments:
Post a Comment