WANAUME WENGI NCHINI UINGEREZA
HULIPIA NGONO
Zaidi ya mwanaume mmoja kati ya 10 wanaelezwa kulipia vitendo vya ngono, utafiti kuhusu tabia za ngono nchini Uingereza.
Asilimia 11 ambao wamefanya hivyo walitembelea maeneo ambapo kuna vivutio vya biashara ya ngono kama vile mjini Bangkok na Amsterdam.
Ripoti kutoka jarida liitwalo Sexually Transmitted Infections inasema tabia za kulipia ngono zina uhusiano na tabia nyingine zilizo hatarishi kama vile ulevi na matumizi ya dawa za kulevya.
Ripoti imeeleza kuwa vijana wadogo kuliko watu wazima wanalipia ngono.
Kati ya wanaume 6,108, asilimia3.6 wamelipia ngono kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na asilimia 1.1 mwaka jana.
Kiongozi wa utafiti huo,Dr.Cath Mercer ameiambia BBC kuwa watu hawa wanaonesha kuwa wana wenzi wengi.
Hata hivyo hali hiyo imeonesha uwepo wa madhara, wanaume waliolipia ngono kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita wako hatarini kukutwa na maradhi ya zinaa na Ukimwi.
Kundi kubwa ambalo hivi karibuni lililipia biashara ya ngono nchini Uingereza ni vijana wa umri wa kati ya miaka 20 na 30,miongoni mwa hawa wengi wao hawajaoa,wakiwa na weledi mzuri,ajira na matumizi ya dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment