FIFA YATISHIA KUIPIGA
MARUFUKU NIGERIA
Chris Giwa |
Shirikisho
la soka ulimwenguni FIFA limetishia kuitimua Nigeria kutoka kwa shirikisho hilo
iwapo Chris Giwa hataacha kujidai kuwa rais wa shirikisho la soka nchini humo.
Shirikisho
hilo limesema Nigeria ina hadi Jumatatu kubadili mambo kwani halimtambui bwana
Giwa kama Rais wa shirikisho la soka nchini humo.
Ikiwa
shirikisho hilo litawekewa marufuku, marufuku hiyo itaondolewa tu iwapo bodi
halali iliyoishidhishwa kushika uongozi Aminu Maigari akiwa rais wake,
itaruhusiwa kuendelea na kazi zake.
Uchaguzi
mpya utahitajika kufanywa haraka iwezekanavyo.
Siku
ya mwisho kwa Giwa kujiondoa kama rais wa NFF ilifikiwa na FIFA Jumatano. Hii
ni baada ya Giwa kukosa kutii makataa ya kuondoka ofisini iliyowekwa na Fifa ya
tarehe 1 Septemba.
Iwapo
Jumatatu itafika na Giwa hatakuwa amejiondoa kama Rais,basi Nigeria ambao ni
mabingwa Afrika hawatashiriki michunao ya kufuzu kwa mechi za kombe la taifa
bingwa Afrika itakayochezwa Afrika Kusini Septemba 10.
Hata
hivyo shirikisho la soka Afrika limesema kwamba ikiwa Super Eagles watakosa
mechi ya kufuzu, basi watatimuliwa kutoka kwa mashindano ya kufuzu kwa kombe
hilo.
Nigeria
ilipigwa marufuku kutocheza soka ya kimataifa kwa siku tisa mwezi Julai sababu
kuu ikiwa serikali kuingilia usimamizi wa soka baada ya Magairi kuondolewa kama
Rais wa shirikisho la soka nchini humo kufuatia uamuzi wa mahakama.
Kamati
ya usimamizi wa NFF ilimuondoa Maigari uongozini kwa kura siku chache tu baada
ya mahakama kuamua vinginevyo. Hata hivyo FIFA haikukubali kitendo hicho na
hapo ndipo Magariri alirejeshewa wadhifa wake tena mwezi Agosti
BBC
BBC
No comments:
Post a Comment