WALIMU
32 KUPATIWA MAFUNZO YA UWALIMU WA MPIRA WA MIGUU MTWARA
Kondo Muhamed |
Baraka Jamali Mtwara
Walimu32
wa shule za sekondari mkoani Mtwara wanatarajia kupata mafunzo ya uwalimu
wa mpira wa miguu ngazi ya awali ili waweze kuwafundisha wanafunzi katika
shule wanazofundisha.
Mwenyekiti
wa chama cha makocha (TAFCA) Mtwara, Kondo Muhamed amesema kuwa kozi hiyo
inatarajiwa kutolewa na mkufunzi anae tambulika na TFF, wa kanda ya kusini
mashariki ya Tanzania, mikoa ya Lindi na Mtwara Hamim Mawazo.
Aidha
amesema lkuwa kozi hiyo inatarajiwa kutolewa kwa walimu kutoka kila
wilaya ya mkoa wa mtwara ili kuweza kuinua kiwango cha soka mkoani hapa kwa
kukuza vipaji vya vijana wadogo wanadogo wa mkoa wa Mtwara.
“Watanzania
kamatunataka kuinua kiwango cha soka ni lazima tuwafundishe walimu wa shule za
msingi na sekondari, ndiko vipaji vya vijana vinaonekana na walimu inatakiwa
wawe tayari kujitolea kuwasaidia vijana hawa ili waweze kulitumikia taifa lao”
alisema mwenyekiti huyo ambae pia alikuwa mchezaji wa timu ya bandari ya
Mtwara.
Pia
aliongeza kuwa kozi hiyo inatarajiwa kuaza kutolewa siku ya tar 13 Septemba
mwaka huu, kwa usajili na wataanza kupewa mafunzo ya darasani na vitendo
septemba 14, ambapo yatatolewa katika shule ya sekondari sabasaba mkoani hapa
pia walimu hao watajilipia ada ya ushiriki ambayo ni sh 30,000.
Kwa
upande wake mratibu wa michezo manispaa ya Mtwara mikindani pia ni mratibu wa kozi
hiyo Said Kaminya, amesema kuwa walimu mkoani Mtwara ni lazima wapatiwe mafunzo
mbalimbali ya michezo ili kuweza kuuletea sifa mkoa wa Mtwara kwani kwa muda
mrefu sasa hakukuwepo na tinu ya mpira wa miguu inayo shiriki ligi kuu, kabla
ya timu ya ndanda kupanda daraja mwaka huu.
“Kama
tunania ya dhati ya kutaka kuendeleza michezo katika mkoa wetu juhudi binafsi
zinahitajika ili kuweza kuuweka mkoa katika chati kitaifa, tumekaa muda mrefu
hakukupe hata timu muja inayo shiriki Ligi kuu kabla ya timu ya ndanda kupanda
daraja msimu huu” alisema Bw Kaminya.
Pia
mkufunzi anaetarajiwa kuendesha kozi hiyo Bwana Hamimu Mawazo akiongea kwa njia
ya simu kutoka jijini Dar es Salaam, amesema kuwa amefurahishwa na walimu hao
kwa kuona umuhimu wa kupewa mafunzo hayo ya ngazi ya awali, kwani itasaidia
kuibua vipaji katika shule zao.
“Ni
kweli kuna walimu 32 nitawapatia mafunzo na ninawapongeza walimu hao kwa kuona
umuhimu wa kupata mafunzo ya ngazi ya awali kwani itawasaidia kuibua vipaji
vyao katika shule zao wanazo fundisha” alisema Mawazo ambae pia ana leseni
ya mpira wa miguu CAF class B.
Ikumbukwe
ya kwamba 26 Mei-Juni 04, walimu 18 wanao fundisha timu za ligi daraja la nne
mjini hapa walipatiwa mafunzo kama hayo na kozi hiyo ikiongozwa na mkufunzi
huyo Bwana Hamimu Mawazo.
No comments:
Post a Comment