ARGENTINA YAICHAPA
UJERUMANI 4-2 MCHEZO WA KIRAFIKI
Kikosi cha Argentina |
Mchezaji
mahiri wa timu ya taifa ya Argentina na pia mchezaji mpya wa Manchester United
ya ligi kuu ya England Angel Di Maria aliitengenezea timu yake magoli matatu
kabla ya kufunga bao lake la nne kwa timu yake ilipowacharaza mabingwa wa dunia
Ujerumani magoli 4-2 katika mchezo uliopigwa dimba la Dusseldorf, nchini
Ujerumani.
Di
Maria, aliyesajiliwa na Manchester United kwa kitita cha pauni milioni £59.7,
alitoa pasi murua kwa Sergio Aguero ambaye bila kigugumizi alipachika goli na
kuiwezesha Argentina kuongoza hiyo ikiwa ni dakika ya 20 ya mchezo.
Mchezaji
mwingine wa timu ya England ya Tottenham, Erik Lamela aliongeza maumivu kwa
mabingwa wa kombe la dunia kwa kupachika goli la pili dakika ya 40 kabla
mchezaji Federico Fernandez pia wa timu ya England ya Swansea kupachika goli la
tatu ni katika dakika ya 47
Di
Maria alihitimisha karamu ya magoli ya Argentina kwa kufunga goli la nne dakika
ya 50 kipindi cha pili cha mchezo.
Ujerumani
iliweza kupunguza kipigo hicho kwa kupachika goli la kwanza kupitia kwa
mchezaji wake Andre Schurrle katika dakika ya 57 ambaye pia ni mchezaji wa
Chelsea ya England na Fernandez alijifunga katika harakati za kuokoa mpira na
hivyo kuinufaisha Ujerumani.
Hadi
mwisho wa mchezo Argentina walitoka kifua mbele kwa ushindi mnono wa 4-2 dhidi
ya mabingwa wa soka wa dunia, Ujerumani. Di Maria hakuweza kucheza katika mchezo
wa mwisho wa fainali za kombe la dunia uliozikutanisha Argentina na Ujerumani,
kutokana na sababu ya kuwa majeruhi, huku Ujerumani ikiibuka mabingwa wapya kwa
kuilaza Argentina 1-0. Mchezo wa Jumatano umekuja siku 52 tangu timu hizo
zilipomenyana nchini Brazil.
Michezo
mingine ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa Jumatano miongoni mwao ni kati ya
England na Norway. England iliibuka kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na
nahodha wake mpya Wayne Rooney kwa njia ya penalti katika dakika ya 68.
Nayo
Urusi iliicharaza Azerbaijan kwa magoli 4-0, huku Marekani ikipata ushindi wa
goli 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech.
BBC
No comments:
Post a Comment