YULE MREMBO WA BURMA AKATAA
KUREJESHA TAJI LAKE
Mrembo Mya Myat Noe |
Mshindi
wa taji la urembo nchini Burma aliyenyang'anywa taji lake wiki iliopita
,amekataa kurudisha taji hilo kwa waandalizi wa mashindano hayo Korea Kusini.
Katika
kikao na wanahabari,Mya Myat Noe amesema kwamba atarudisha tu taji hilo lenye
thamani ya dola 100,000, ikiwa ataombwa msamaha na waandalizi wa mashindano
hayo.
Bi
May alishinda mashindano ya Miss Asia Pacific World mwaka 2014 iliyofanyika
mwezi Mei mjini Seoul.
Wiki
jana waandalizi walimshtumu kwa kukosa shukrani na kutokuwa mkweli.
Bi
May ni mshindi wa kwanza wa shindano hilo nchini Burma , kulingana mwandishi wa
BBC Jonah Fisher.
Mrembo
huyo alidaiwa kutoroka na taji hilo, madai ambayo ameyakanusha.Bi May aliwaambia wanahabari kuwa alilazimishwa kudanganya kuhusu umri wake na waandalizi hao pia walimshurutisha kuwekwa matiti bandia.
Hata hivyo amekana madai ya kuwa alitoroka na taji hilo akisema kuwa aliabiri ndege kuelekea Myanmar bila kufahamu kuwa alikuwa ashavuliwa taji hilo.
Waandalizi walidai kuwa mwanadada huyo aliwadanganya na kuwadharau, ila hawakutoa maeleo zaidi.
Baadaye ilifahamika kwamba kulikuwa na mtafaruku kati ya mamake May na waandilizi hao kuhusiana na vipi Bi May anaweza kusimamiwa .
BBC
No comments:
Post a Comment