Saturday, September 20, 2014

LIGI KUU VODACOM: MABINGWA AZAM FC WAANZA KIDEDEA, YANGA HOI MORO


LIGI KUU VODACOM, VPL, Msimu wa 2014/15 imeanza rasmi hii Leo na Mabingwa Azam FC kuanza kwa ushindi wa Bao 3-1 dhidi ya Polisi ya Morogoro huko Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam wakati Yanga wakisulubiwa 2-0 na Mtibwa Sugar huko Jamhuri, Morogoro.
Bao za Azam FC zilifungwa na Didier Kavumbagu, Bao 2, na Aggrey Moses na Bao pekee la Polisi lilifungwa na Bakari.
Huko Morogoro, Bao za Mtibwa Sugar zilipigwa na Mussa Mgosi, Dakika ya 15, na Ame Ali, Dakika ya 82.
Jumapili, Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam itakuwepo Mechi ya ‘Wapwa’ wakati Simba itakapocheza na Coastal Union.
RATIBA
Septemba 20
Azam FC 3 Polisi Moro 1
Mtibwa Sugar 2 Yanga 0
Stand United 4 v 1 Ndanda FC
Mgambo JKT 1v  0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 0 v 1Tanzania Prisons
Mbeya City 0 v 0 JKT Ruvu
Septemba 21
Simba v Coastal Union [Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam]

No comments: