Monday, September 22, 2014


Alessandro Florenzi akifunga bao
Alessandro Florenzi akienda jukwaani

Alessandro Florenzi akikumbatiana na bibi yake

Alessandro Florenzi akirejea uwanjani
Mshambuliaji wa AS Roma ya Italia, Alessandro Florenzi baadaya ya kufunga bao aliamua kupanda jukwaani na kumkumbatia bibi yake mwenye umri wa miaka 82.
Ilikuwa ni mechi kati ya AS roma dhidi ya Cagliari na wakashinda kwa mabao 2-0, yote yakiwa yamefungwa na mshambuliaji huyo.

Mara baada ya kufunga mshambuliaji huyo alipanda kasi kwenda juu ya jukwaa na kumkumbatia bibi huyo.
Referee wa mchezo huo alimzawadia kadi ya manjano kwa kitendo hicho.

Huo ulikuwa ni ushindi mwingine wa AS Roma baada ya kuwa imeiadhibu kwa mabao 5-1 timu ya CSKA Moscow katika Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments: