BAYERN MUNICH AYAIBANJUA MAN CITY UEFA, BACELONA NAYO YATAKATA
Mechi
zilizochezwa usiku wa kuamkia leo za Klabu Bingwa barani ulaya ambapo
Manchester City walianza vibaya michuano hiyo baada ya kupata kichapo cha goli
moja bila majibu kutoka kwa wenyeji wao Bayern Munich ya Ujerumani.
Goli la
Bayern Munich lilifungwa na Jerome Boateng katika dakika 90Wakati Man City wakiiadhibiwa ugenini na Bayern Munich, wenzao Chelsea wakiwa nyumbani Stamfode Bridge walitoka na sare ya goli moja kwa moja na Schalke 04.
AC Roma ya Italia wao waliiadhibu CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 5 -1 huku Ajax na Paris St. Gamaine ya Ufaransa zikitoka sare ya moja kwa moja.
Bacelona wao waliamua kuushikisha adabu Apoel ya Syprus kwa kuifunga goli moja bila majibu wakati FC Porto ya Ureno wakifungulia mvua ya magoli iliyoambatana radi pale ilipowanyeshea wapinzani wao Bate Borisov ya Belarus kwa jumla ya magoli 6 bila majibu.
Matokeo mengine NK Maribor ya Slovenia ilitoka sare ya 1 - 1 na Sporting Lisbon ya Ureno huku Athletic Bilbao ya Hispania zikitoka uwanjani bila kufungana na Shaktar Donetsk ya Ukraine.
No comments:
Post a Comment