MREMBO APOKONYWA TAJI
KUTOKANA NA UJEURI WAKE
May Myat Noe |
Mshindi
wa mashindano ya taji la Miss Asia Pacific World, May Myat Noe, amevuliwa taji
lake akisemekana ni mjeuri, hana hadhi na hastaili taji hilo.
May
Myat Nwoe alivishwa taji lake mwezi Mei baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekwa
matiti bandia kufuatia ombi la waandalizi wa mashindano hayo wa Korea.
Baadaye
walimlaumu wakisema hataki kushirikiana nao na sasa wanataka aombe radhi na pia
arejeshe taji alilovishwa.
Waandalizi
walisema hawajafurahishwa na kitendo cha msichana huyo kumpeleka mamake nchini
Korea Kusini.
May
Myat Noe, mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka Burma, sasa anaripotiwa
kutoweka na taji alilovikwa aliposhinda mwaka jana.
Msemaji
wa waliodhamini taji hilo anasema msichana huyo wa miaka 18 alitoweka baada ya
kufahamishwa uamuzi huo wa kumpokonya taji hilo wiki jana.
BBC
imefahamishwa kwamba waandalizi wa shindano hilo pamoja na mamake msichana huyo
walitofautiana kuhusu usimamizi wake.
Shirika
lilioandaa shindano hilo, limesema kuwa Bi May alidanganya na kwamba hana
heshima kwa waandalizi wa shindano hilo.
Lilisema
kukosa heshima kwake ni moja ya sababu za kumpokonya taji lake.
Kadhalika
shirika hilo lilisema kuwa msichana huyo, aliyekuwa amepata mikataba ya kufanya
rekodi ya miziki pamoja na kuigiza, alitoroka na taji lake lenmye thamani ya
dola 100,000.
Mwandishi
wa BBC Jonah Fisher anasema kuwa mamake May alionekana kutaka kumsimamia
msichana wake lakini chini ya masharti ya shindano hilo, mshindi anapaswa
kusimamiwa na waandalizi.
Inadhaniwa
Bi May amerejea nchini Burma.
BBC
No comments:
Post a Comment