Friday, August 29, 2014


Mji wa Noiva do Cordeiro
Mji mmoja nchini Brazil ambao una wanawake watupu, wengi wakiwa mabinti warembo  umetoa wito wa kutaka vijana wa kiume - ambao bado ni makapera (yaani single).
Kwa mujibu wa tovuti ya Metro, mji huo uitwao Noiva do Cordeiro, una watu 600, ambao wote ni wanawake. Watoto wa kiume wanaozaliwa katika mji huo hutakiwa kuondoka wakitimiza umri wa miaka 18, na waume kadhaa wenye wake zao huko, hutakiwa kwenda mjini humo siku za wikendi tu.
Wanawake vijana katika mji huo sasa wamechoshwa na kutokuwepo na wanaume na wametoa wito kwa wanaume makapera kujitokeza
"Hapa, wanaume pekee tunaokutana nao, ama wameoa, au ni ndugu zetu, kila anaye kuja hapa ni binamu. Sijapata kubusu mwanaume kwa muda mrefu," amesema Nelma Fernandes, 23, akizungumza na gazeti la Mirror."Sote tunaiota siku ambayo tutakutana na mwanaume na kupendana naye na kufunga ndoa. Lakini tunapenda kuishi hapa, na hatutaki kuuhama mji wetu kwenda kutafuta waume."
Mji huo wa 'ajabu' ulianzishwa na Maria Senhorinha de Lima, aliyekimbia ndoa ya kulazimishwa na pia kubandikwa jina la mzinzi.
Warembo wa mji wa Noiva do Cordeiro
Wanawake wengine waliotengwa na jamii waliungana naye na mji wa Noiva do Cordeiro
Lakini kabla makapera hamjakata tiketi kwenda huko, kuna tahadhari:
"Utafuata tunalosema na kuishi kwa sheria zetu," anasema Nelma. "Kuna vitu vingi ambavyo wanawake hufanya vizuri zaidi kuliko wanaume. Mji wetu ni mzuri, una utaratibu mzuri, na una amani zaidi kuliko kama ungekuwa unaongozwa na wanaume.
"Na pia mara zote kuna muda wa umbea, na vilevile kujaribu nguo na kutengeneza nywele na kucha."
Taarifa na picha kutoka: Metro.co.uk

No comments: