Thursday, August 7, 2014

Wanaume 12 wamejikuta wakilazimishwa kutaihiriwa bila ridhaa yao hivi karibuni nchini Kenya. Wanaume hao wa jamii za Wajaluo, Turkana, Iteso na Luhya walivamiwa katika mji mdogo wa Moi Bridge, huko Rift Valley na kulazimishwa kufanyiwa tendo la tohara wikiendi iliyopita baada ya fununu zilizokuwa zikizunguka kuwa hawajatahiriwa.

Kwa mujibu wa mtandao Daily Post nchini humo ulioripoti jumatatu tarehe 4, wake za wanaume hao 12 waliamua kuvujisha siri za ndani za waume zao baada ya kulalamika kuwa hawaridhishwi katika tendo la ndoa na kwamba kuna hali ya uchafu mwingi katika maumbile ya waume zao.

Wanaume hao ambao wengi wao ni madereva na makuli walijikuta katika wakati mgumu baada ya kulazimishwa kushusha suruali zao hadharani na kuanza kufanyiwa upasuaji huo mbele ya kadamnasi bila ganzi ili kupunguza maumivu.

Mwanamke mmoja aliyejitambulisha kama Ann Njeri, aliliambia gazeti hilo kuwa anafuraha kwamba mumewe amefanyiwa tohara kwani sasa ataanaza kufurahia uwezo mpya na kwa usafi katika tendo la ndoa katika ndoa yake.

Wanaume waliotekeleza kitendo hilo walidai kuwa shughuli hiyo itaendelea katika eneo hilo mwenzi mzima wa Agosti, mwezi ambao ni msimu wa tohara, ili kuhakikisha wanume wote wana kamilika kutoka kwenye uvulana kuwa wanaume.

Watahiriwa hao 12 walipewa kiasi cha shilingi 3000 za Kenya (sawa na shilingi za Kitanzania 56,584) kwaajili ya matibabu na chakula chenye virutubisho muhimu, ili kupona haraka.  Wakati huo huo zaidi ya wanaume 50 ambao hawajatahiriwa wanaoishi katika mji wa Daraja la Moi wamepiga kambi katika kituo cha polisi wakihofia kutahiriwa kwa nguvu kama marafiki zao.

No comments: