Hamis Juma na mkewe Cecilia Hamis |
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita nyumbani kwake, mwanamke
huyo alisema alibaini hilo wiki mbili zilizopita.
“Nililigundua
hilo wiki mbili zilizopita. Nakumbuka ilikuwa usiku nikiwa nimelala, nikamsikia
mbwa mmoja (kati ya wawili) analia. Niliamka kwenda kuangalia ili kujua sababu,
kufika nikawasha tochi ya simu, nilishangaa sana kumwona mume wangu yuko naye
anafanya mapenzi.
“Nilimuuliza anachokifanya, akasema
anammalizia shida zake kwa kuwa hakuna mbwa wa kiume wa kumsaidia,” alisema
mwanamke huyo.
Akiendelea kumlalamikia mume wake kwa
madai hayo mazito, mama huyo alisema:
“Siku iliyofuata usiku tena, nikiwa
nimelala nilimsikia mbwa akilia, nikaamka. Safari hii niliambatana na watoto
wangu, tukaenda nje, kufika tukamshuhudia mume wangu akifanya tukio kama la
jana yake, nilipomuuliza akanipa majibu yaleyale kwamba anammaliza shida zake
mbwa huyo.”
Akaendelea: “Hawa
mbwa waliletwa wawili wakiwa wadogo kabisa na wote ni majike na tangu
walipoletwa sijawahi kumwona mbwa dume hata siku moja kwani mara nyingi
tunawafungia kwenye banda lao.
“Na tangu mume wangu aanze mchezo huo
huyo mbwa mmoja mweusi amenawiri kupita kiasi, naamini amempa mimba.”
Mwanamke huyo alisema kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo,
aliamua kuwaeleza majirani ambao nao walimshauri aende kuripoti kwa mjumbe wa
eneo hilo.
Akizungumzia swala hilo, Mjumbe wa Shina Na. 26, Majoe Mjimpya,
Mbaruka Nyamaishwa alikiri kupokea malalamiko hayo kutoka kwa mwanamke huyo
akamshauri kuyapeleka kwenye Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Habari zaidi zinawekwa wazi kwamba, majirani nao walipoona
mwanamke huyo anachelewa kwenda polisi, wao walimsomba na kwenda naye ambapo
walitoa taarifa katika Dawati la Jinsia.
Mkuu wa dawati hilo, Koplo Golbert aliongozana na walalamikaji
hao hadi nyumbani kwa mdaiwa ambapo alimkagua mbwa huyo na kuwaamuru wanandoa
hao kuripoti kwenye kituo hicho cha polisi bila kukosa jana Jumatatu saa 3
kuonana na mkuu huyo na uchunguzi kuendelea.
Uwazi lilimuuliza swali moja mwanamke huyo, ni kwa nini anasema
aliamka na kutoka nje usiku bila kueleza mumewe anakuwa wapi muda huo kwani
hakuonyesha kushangaa kutomwona kitandani?
Anajibu: “Tulitengana
vyumba kwa sababu ya ugomvi wa kifamilia.”
Alipoulizwa
mume wa mwanamke huyo kuhusu madai mazito ya mkewe alisema:
“Mimi sijawahi kufanya kitendo hicho
na mbwa ila nahisi mke wangu na hawa majirani wa hapa wananitengenezea hilo
tukio ili nikafungwe jela maisha, halafu wao waweze kuchukuwa mashamba yangu
kwani ndani ya ndoa yangu kumekuwa na ugomvi wa mara kwa mara.”
Uwazi lilitilia shaka uwezekano wa mbwa kunasa mimba ya
binadamu, hivyo lilimsaka daktari mmoja wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)
na kumuuliza kuhusu madai ya mwanamke huyo.
Msikie: “Mh!
Binadamu kumpa mimba mbwa haiwezekani. Binadamu anaweza kumpa mimba sokwe, kwa
mbali sana nyani. Lakini si mbwa.
“Ila kama huyo mama anasema hivyo,
mbwa akapimwe na ikibainika ni kweli basi yatakuwa maajabu ya dunia maana dunia
ina mambo yake.”
GPL
No comments:
Post a Comment