EVODIUS
MTAWALA, AACHIA NGAZI TFF
Evodius Mtawala |
Mkurugenzi wa wa Vyama na Masuala ya Kisheria
katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Evodius Mtawala, amelazimika kuachia
ngazi kutokana na sababu mbalimbali.
Taarifa zinaeleza kuwa Mtawala ambaye aliwahi
kuwa Katibu Mkuu wa Simba, alikuwa na
hali ya kutokuelewana na uongozi wa shirikisho hilo na ndiyo chanzo kikubwa cha
kumfanya ang'atuke TFF.
Katibu Mkuu wa TFF, Selestine Mwesigwa,
alithibitisha kuachia ngazi kwa Mtawala lakini akasema ni kutokana na sababu
mbalimbali za taaluma yake ya uanasheria.
“Ni kweli Mtawala hataendelea kufanya kazi TFF
lakini ameamua kuchia ngazi mwenyewe kutokana na sababu mbalimbali alizodai
kwamba ni kujikita na taaluma yake zaidi kwa sasa, lakini mambo mengine juu ya
hilo yatabaki kuwa siri baina yake na mwajiri wake.
“Ila mpaka makubaliano ya mwisho yalieleza
kuwa itakapofika mwisho wa mwezi wa nane (jana 31, Agosti) atakuwa tayari
ameshakabidhi ofisi na kuendelea na masuala ambayo alidai anahitaji kujikita
zaidi kulingana na taaluma yake,” alisema Mwesigwa.
Mtawala amedumu kwenye wadhifa huo kwa miezi
nane tu tangu alipoteuliwa Desemba 24, mwaka jana chini ya uongozi wa rais
mpya, Jamal Malinzi.
No comments:
Post a Comment