MKE NA MUME WAFA PAMOJA BAADA YA KUISHI MIAKA 62
Kisa
kimoja ambacho kimedhibitishia wengi baada ya wapenzi wawili waliooana na
kuishi pamoja kwa takriban miaka 62 walipoaga dunia pamoja.Don na Maxine Simpson walikuwa wakazi wa mji wa Bakersfield, ulioko jimbo la California, Marekani waliaga dunia saa nne baada ya kushikana mikono hospitalini na kuahidiana penzi lao halitafifia kamwe hata mauti iwapate.
Walikuwa wamelazwa hospitalini kufuatia hali duni ya afya inayotokana na umri wao mkubwa.
Lakini punde alipoaga Maxine na mwili wake ukaondolewa chumbani walikokuwa wamelazwa pamoja na mumewe Don, zilipata saa nne tu uchungu ulipomzidi Don na akakata roho iliwaendelee kupendana na mkewe ahera.
Mjukuu wao Melissa Sloan aliiambia runinga ya KERO-TV Kuwa Don alimhusudu sana nyanya yake yaani Maxine tangu alipomtupia jicho mnamo mwaka wa 1952 walipokutana katika mashindano ya Bowling.
Wapenzi hao wawili waliooana mwaka huohuo na hawajawahi kuachana tangu hata katika mauti.
''Babu yangu alikuwa anatamani kuishi na nyanya yangu na hata baada ya wawili hao kuanza kuugua kutokana na umri wao mkubwa waliwaomba wasimamizi wa hospitali walimolazwa wasiwatenge.''
Don alikuwa na miaka 90 huku mke wake akiwa na miaka 87.
''Babu yangu alihudumu kama mwanajeshi katika jeshi la Marekani naye bibi alikuwa ni muuguzi haswa walipokuwa huko Ujerumani ambapo waliwahi kuishi kwa muda mrefu.''alisema mjukuu wao Melissa.
Wamemuacha nyuma mtoto mmoja wa kiume na wajukuu watano.
BBC
No comments:
Post a Comment