AFUKUZWA KAZI KWA KUMTONGOZA
MWANAMKE WA KIHINDI.
Kijana mmoja aliyekuwa akifanya kazi ktk mgodi wa
Bulyanhulu wa Barrick, amefukuzwa kazi
wiki iliyopita baada ya kuonyesha hisia zake kwa binti wa kihindi raia wa south
africa, ambaye naye ni mtaalam wa mgodi ule,walipeana namba za simu, kijana wa
watu akatupa ndoana kujaribu bahati yake, mambo yakamgeuka,binti akashtaki kwa
makaburu wa mgodini, kesi ikaitishwa, hukumu ikatoka kuwa kavunja sheria kwa
kumnyanyasa kimapenzi, kazi ikaisha
Ajabu ni
kuwa weusi huwa wanatongozana lakini hakuna kesi, wala kufukuzwa kazi, lakini
baada ya mweusi kumtongoza mweupe, kibao kikageuka kuwa ni unyanyasaji wa
kimapenzi, tukio hili limepandisha hasira watu, wakijiuliza kwa nini mtu
abaguliwe ndani ya ardhi yake na wageni?
No comments:
Post a Comment