Wednesday, July 9, 2014

SCOLARI AJIBEBESHA MZIGO WA LAWAMA ASEMA JANA NI SIKU MBAYA SANA KATIKA MAISHA YAKE
Felipe Scolari ( Tumefungwa saba kweli? inaniuma sana)
MARA baada Jana Usiku Wenyeji Brazil kupewa kisago kikubwa katika Historia ya Kombe la Dunia baada Germany kuwabamiza Bao 7-1 katika Mechi ya Nusu Fainali, Kocha wa Brazil ameeleza kuwa ni ‘Siku mbaya sana katika maisha yake’ na kukubali lawama zote.
Kwenye Mechi hiyo, Ndani ya Nusu Saa, Germany walikuwa mbele kwa Bao 5-0.
Scolari, ambae alishinda Kombe la Dunia na Brazil Mwaka 2002, alisema: “Nitakumbukwa kama Kocha aliefungwa 7-1 lakini nilijua hatari yake nilipokubali kazi hii. Mtu anaechagua Kikosi, mbinu ni mimi. Lilikuwa chaguo langu.“
Scolari ameeleza kipigo hicho ni ‘janga!’
Alisema: “Ujumbe wangu kwa Watu wa Brazil ni kuwaomba watusamehe kwa uchezaji huu.”
“Naomba radhi kwamba hatukuweza kufika Fainali na tutajaribu kushinda Nafasi ya Tatu. Bado tunacho kitu cha kupigania.”
Hii ni mara ya kwanza tangu 1938 kwa Brazil kupoteza Nusu Fainali ya Kombe la Dunia na ni kipigo kikubwa kingine kwa Brazil  Mwaka 1920 walipochapwa 6-0 na Uruguay
Scolari amekataa kuchukulia kukosekana kwa Staa wake Neymar na Nahodha wake Thiago Silva kuwa ndio sababu na kueleza: “Tusitafute kisingizio kwa Neymar. Tulijaribu kadri ya uwezo wetu na tumekutana na Kikosi cha Germany kilicho bora. Tulishindwa kujizoa baada kuwa nyuma. Hata Wajerumani hawawezi kukuelezea nini kilitokea lakini ni sababu ya ufundi wao na lazima uheshimu hilo!”
Katika mchezo huo Thomas Muller ndie aliefungua milango na kufuatia Miroslav Klose aliefunga Bao la Pili na sasa kushika Rekodi ya kuwa Mfungaji Bora katika Historia ya Kombe la Dunia akiwa na Bao 16.
Dakika moja baadae, Toni Kroos akafunga Bao la 3 na la 4 kufuatia Dakika 2 baadae.
Sami Khedira akafunga Bao la 5 katika Dakika ya 29.
Kipindi cha Pili, Andre Schürrle akafunga Bao 2 na kuifanya Germany iongoze 7-0.
Bao pekee la Brazil lilifungwa Dakika ya 90 na Oscar.
Germany watacheza Fainali hapo Jumapili na Mshindi wa Mechi kati ya Argentina na Netherlands wanaocheza  Usiku wa leo.
Brazil watacheza Jumamosi na Timu itakayofungwa Nusu Fainali ya Jumatano kwenye Mechi ya kusaka Mshindi wa Tatu.

No comments: