Thursday, July 3, 2014

FIFA YATAJA MAREFA ROBO FAINALI YATAFAKARI MCHEZAJI MMOJA WA AKIBA WA ZIADA KUINGIZWA DAKIKA ZA NYONGEZA 30

FIFA imetangaza Marefa wa Mechi mbili za Robo Fainali za Kombe la Dunia za huko Brazil zitalazochezwa Ijumaa kati ya France v Germany na Brazil v Colombia.
Nestor Pitana atasimamia Mechi ya kwanza ya Ijumaa kati ya France v Germany na hii itakuwa ni Mechi ya 4 kwa Refa huyo kutoka Argentina kuchezesha huko Brazil.
Pitana, mwenye Miaka 39, alichezesha Mechi za Makundi huko Brazil kati ya Russia na Korea Republic, USA na Portugal na Honduras dhidi ya Switzerland.
Mechi ya Wenyeji Brazil na Colombia itachezeshwa na Refa wa Spain Carlos Velasco.
Velasco, mwenye Miaka 43, ameshasimamia Mechi 2 huko Brazil ambazo ni zile za Makundi kati ya Uruguay na England na ile ya Bosnia and Herzegovina dhidi ya Iran.
FIFA YATAFAKARI MCHEZAJI MMOJA WA AKIBA WA ZIADA KUINGIZWA DAKIKA ZA NYONGEZA 30
Jopo la Washauri wa Masuala ya Makocha la FIFA linatafakari kutoa mapendekezo kwa FIFA kuruhusu idadi ya Wachezaji wa Akiba wanaotoka Benchi na kuruhusiwa kucheza iwe Wanne badala ya Watatu wa sasa.
Lakini Jopo hilo linataka Mchezaji huyo wa Nne atakaeruhusiwa awe anaingizwa wakati wa Nyongeza za Dakika 30 baada ya Timu kwenda Sare katika Dakika 90.
Kocha wa zamani wa Liverpool, Gerard Houllier, ambae ni mmoja wa Wajumbe wa Jopo hilo amesema: “Ni wazo zuri ambalo tutalipeleka kwenye Vikao vya Kutunga Sheria FIFA!”
Houllier, ambae pia aliwahi kuwa Kocha wa France, amefafanua kuwa kuruhusu Mchezaji wa 4 kuingia kwenye Dakika za Nyongeza 30 itasaidia kupunguza athari za Wachezaji kubanwa na Musuli wakati huo na kuzipa nafuu Timu.
Pia, Houllier amesisitiza Wachezaji wanaotoka Benchi wana mchango mkubwa wa kubadilisha matokeo ya Mechi kwani huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia Wachezaji waliotoka Benchi na kuingizwa wamefunga Bao 29 na kuvunja Rekodi ya Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2006 huko Germany walipofunga Bao 23 na bado Fainali hizi ina Mechi 8 hazichezwa.
Houllier amesema: “Wachezaji wa Akiba wana umuhimu mkubwa kwa sababu wanaingia freshi na akili mpya. Karibu robo ya Magoli yamefungwa kwenye Robo Saa ya mwisho huko Brazil. ”
Baadhi ya Magoli hayo ni mchango wa Klaas-Jan Huntelaar alipoingizwa Dakika ya 76 kutoka Benchi na kuisaidia Netherlands kwa kumpasia Wesley Sneijder Dakika ya 88 na kusawazisha na kisha yeye mwenyewe kufunga Bao la Pili na la ushindi kwa Penati ya Dakika ya 94 walipoibwaga Mexico 2-1.
Majuzi Jumatatu, baada ya Kipa wa USA Tim Howard kuizuia Belgium na kutoka Sare nao 0-0 katika Dakika 90, akaingizwa Romelu Lukaku ambae, katika Dakika za Nyongeza 30, alimpasia Kevin De Bruyne aliefunga Bao la kwanza na yeye mwenyewe kupiga Bao la pili na Belgium kuibwaga USA 2-1.
Mwaka 2012, FIFA iliwahi kuyakataa mapendekezo ya aina hii hii ya kuongeza Wachezaji wa Akiba kuruhusiwa kucheza kuwa Wanne lakini safari hii Houllier anaamini yatapitishwa.
KOMBE LA DUNIA
RATIBA
ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
France v Germany [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro
2300
Brazil v Colombia [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão, Fortaleza
JUMAMOSI, JULAI 5, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina v Belgium [59]
ROBO FAINALI
Nacional, Brasilia
2300
Netherlands v Costa Rica [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova, Savador
NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Mshindi 57 v Mshindi 58 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão, Belo Horizonte
JUMATANO, JULAI 9, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Mshindi 59 Mshindi 60 [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians, Sao Paulo
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Aliefungwa 61 v Aliefungwa 62
MSHINDI WA 3
Nacional, Brasilia
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2200
Mshindi Mechi 61 v Mshindi Mechi 62
FAINALI
Estadio do Maracanã, Rio de Janeiro

No comments: