Thursday, July 3, 2014

YANGA YATOA OFA KUONA KOMBE LA DUNIA PIA KUKUTANA NA MAXIMO

KLABU ya Yanga Leo hii imetoa mwaliko maalum kwa Wananchama na Wapenzi wake hapo Ijumaa kwenda kushuhudua Mechi za Robo Fainali za Kombe la Dunia na pia kuonana na Kocha wao mpya, Marcio Maximo.
Yanga imesema Ijumaa Jioni Wapenzi na Wanachama wao wajumuike kwenye Kumbi za Sinema za Quality Center Jijini Dar es Salaam kushuhudia Mechi za Kombe la Dunia kati ya France na Germany na kisha Brazil v Colombia.
Pia itakuwepo fursa ya kujiandikisha Kadi Mpya za Uanachama kutoka Benki ya Posta na vile vile kuonana na Kocha mpya Marcio Maximo.
Kwenye hafla hiyo, Kundi la Ze Comedy litakuwepo.
Hivi Juzi, Kocha kutoka Brazil, Marcio Maximo, na Msaidizi wake, Leonadro Neiva, walisaini Mkataba wa Miaka miwili kuifundisha Yanga.
Maximo aliwahi kuwa Tanzania kama Kocha wa Timu ya Taifa kuanzia Mwaka 2006 hadi 2010 na kuleta mapinduzi na mafanikio makubwa ikiwemo kucheza Fainali za CHAN.
Vile vile, Maximo amefanikisha kwa Kiungo Mshambuliaji kutoka Brazil Andrey Macrcel Ferreira Coutinho kutua Klabuni Yanga kwa Mkataba wa Miaka miwili na amekuwa kivutio kikubwa kwenye Mazoezi ya Yanga.
Maximo na Msadizi wake Neiva, kwa Siku kadhaa sasa, wamekuwa wakiendesha Programu kali ya Mazoezi ya mara mbili kwa Siku wakianzia huko Coco Beach Asubuhi na Jioni kuwa Uwanja wa Bandari College, Tandika huku wakishuhudiwa na Maelfu ya Washabiki wao.
Wachezaji wanaoshiriki Mazoezi hayo ni pamoja na Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez", Juma Abdul, Swaleh Abdallah, Rajab Zahir, Mbuyu Twite, Salum Telela, Omega Seme, Hassan Dilunga, Said Bahanuzi, Andrey Coutinho, Hussein Javu, Nizar Khalfani na Jerson Tegete.

No comments: