AVEVA AANZA KAZI KWA KUUNDA KAMATI ZA MASHINDANO NA SOKA LA VIJANA.
Rais wa Simba SC, Evans
Aveva (katikati) akizungumza na Waandishi wa Habari
|
RAIS mpya wa Simba SC
amemteua Zacharia Hans Poppe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
klabu hiyo, huku Makamu wake akiwa ni Kassim Mohammed Dewji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana wa leo makao makuu ya klabu, Msimbazi, Dar es Salaam Aveva aliwataja Wajumbe wa Kamati hiyo kuwa ni Said Tuliy, Musley Al Ruwaih, Crescentius Magori na Dk Roadney Chiduo

Aveva pia ameunda Kamati
mbili zaidi, ya Soka ya Vijana itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Said Tuliy,
Ally Suru, Patrick Rweyemamu, Mulamu Nghambi, Madaraka Suleiman na Amina Poyo.
Kamati ya Mashindano Mwenyekiti wake atakuwa Mohammed Nassor, Makamu Iddi Kajuna na Wajumbe Jerry Yambi, Hussein Simba na Mohammed Omar.
Aveva amesema pia baada ya kikao cha kwanza cha Kamati ya Utendaji jana, Mohammed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah wameteuliwa katika Kamati ya Utendaji.
Aveva amesema kikao cha jana pia kiliamua kuwasimamisha uanachama, wanachama 69 waliokwenda Mahakamani kupinga uchaguzi wa klabu hiyo mwishoni mwa mwezi uliopita.
Amesema hatima ya wanachama hao, pamoja na ya mwanachama mwingine maarufu, Michael Wambura aliyeenguliwa kwenye uchaguzi kwa kosa kama hilo, itaamuliwa katika Mkutano Mkuu Agosti 3, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment