HIVI
WAAFRIKATUMELAANIWA KOMBE NA DUNIA? NIGERIA NA ALGERIA NAO NJE
Pamoja na Ugermany kuendeshwa mchakamchaka na Algeria katika Mechi ya Raundi ya Pili ya Kombe la Dunia iliyochezwa Jana Usiku huko Estadio Beira-Rio Mjini Porto Alegre Nchini Brazil na kuhitaji Dakika 120 lakini imefanikiwa kushinda Bao 2-1 dhidi ya Algeria.
Matokeo hayo yameiacha Afrika isiwe na hata Timu moja baada ya mapema Jana Nigeria kufungwa 2-0 na France na kutolewa nje ya Mashindano haya.
Kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil, Timu nyingine za Afrika zilizoshiriki na kutupwa nje Hatua ya Makundi ni Ghana, Cameroon na Ivory Coast.
Hadi Dakika 90 Bao zilikuwa 0-0 na mara nyingi kwenye muda huo, Germany walionekana kupwaya, wazito na kuendeshwa puta na Algeria ambayo ilikosa nafasi kadhaa.
Lakini ndani ya Kipindi cha Kwanza cha Dakika za Nyongeza 30, Dakika 2 tu tangu kianze, Andre Schurrle akaifungia Bao Germany na Mesut Ozil kuongeza la Pili Dakika ya 119 na kuwafanya waongoze 2-0.
Algeria walipata Bao lao moja mwishoni, Dakika ya 120, kupitia, Abdelmoumene Djabou
Germany, ambao wanasaka Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 1990, sasa wametinga Robo Fainali kwa mara ya 17 kati ya 18 ya Fainali za Kombe la Dunia walizocheza.
Kwenye Robo Fainali, Germany watakutana na France ambayo mapema Jana Usiku waliifunga Nigeria Bao 2-0.
Kwenye mchezo huo Bao zote zilifungwa Kipindi cha Pili na la kwanza kwenye Dakika ya 79 kwa Kichwa cha Paul Pogba baada ya Kipa Enyeama kushindwa kuicheza Krosi na kumkuta Pogba aliemalizia kilaini.
Bao la Pili lilifungwa Dakika ya 91 na ni la kujifunga mwenyewe Joseph Yobo baada ya Krosi ya chini ya Mathieu Valbuena kuchinjwa na Antoine Griezmann na Mpira kumgusa Yobo na kutinga wavuni.
Kufuatia kuondolea katika michuano hiyo kocha wa
Nigeria Stephen keshi ametangaza kujiuzuru huku Joseph Yobo akitangaza kustaafu kuchezea timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment