Monday, July 14, 2014

WACHAMBUZI WA SOKA WASEMA NI AIBU KUBWA KWA MESSI KUWA  MCHEZAJI BORA KOMBE LA DUNIA

JANA Usiku Argentina ilichapwa Bao 1-0 na Germany kwenye Fainali ya Kombe la Dunia na Kombe kwenda Germany lakini Nahodha wao Lionel Messi alizoa Mpira wa Dhahabu, ikimaanisha yeye ndio alikuwa Mchezaji Bora wa Fainali za Kombe la Dunia zilizochezwa Brazil.
Mbali ya Messi kutwaa Tuzo hiyo, wengine waliozoa Tuzo binafsi kwenye Fainali hizo ni Straika wa Colombia, James ‘Bond’ Rodriguez, alietwaa Buti ya Dhahabu kwa kuwa Mfungaji Bora, Kipa wa Germany, Manuel Neuer, alietwaa Glovu ya Dhahabu na Paul Pogba wa France alietunzwa kama Mchezaji Bora Kijana.
Lakini baadhi ya Wachambuzi wamekuja juu na kudai kumpa Mpira wa Dhahabu Messi ni ‘aibu kubwa.’
Wengi walishangazwa na uteuzi huo wa FIFA wakidai Messi, mwenye Miaka 27, alionekana mchovu na chini ya kiwango kwenye Mechi nyingi za Mashindano hayo huko Brazil.
Mmoja wa Wachambuzi hao, Stan Collymore, Mchezaji wa zamani wa Liverpool, hakutafuna maneno na kudai, Messi, licha ya kufunga Bao 4 kwenye Fainali hizo na kuisaidia kuifikisha Timu yake Fainali, hakustahili na wapo wengi walifaa kupewa Tuzo hiyo.
Collymore alisema: “Kwenye Fainali uchezaji wake ulikuwa hafifu. Tumemwona mara 3 au 4 sasa akicheza ovyo chini ya kiwango ukiondoaya Mipira miwili au mitatu aliyokokota na kukimbia nayo!”
Aliongeza: “Hii ni aibu kubwa kumpa yeye Mpira wa Dhahabu. Ukiwaangalia Wachezaji kama James Rodriguez, au hata Mchezaji wa Chile Alexis Sanchez na Manuel Neuer, wao wanastahili zaidi!”
Alimalizia: “Hata kwenye hii Fainali hii hakuwa Mchezaji Bora wa Argentina, kwangu Kura inakwenda kwa Javier Mascherano!”
Katika Fainali ya jana iliyochezwa huko Estadio Maracana Jijini Rio de Janeiro na Germany kuibuka Mabingwa wa Dunia baada kuifunga Argentina Bao 1-0 kwa Bao la ndani ya Dakika za Nyongeza 30 la Dakika ya 113 la Mario Gotze alietokea Benchi na kuingizwa Dakika ya 88.
Hii ni mara ya kwanza kwa Nchi kutoka Ulaya kutwaa Kombe la Dunia huko Marekani ya Kusini lakini Mashabiki wa Brazil, ambao wamelikosa Kombe hilo Nyumbani kwao baada kutandikwa 7-1 na Germany kwenye Nusu Fainali, walishangilia ushindi wa Germany kwa vile Hasimu wao mkubwa ni Argentina.
Kwenye Mechi hiyo Lionel Messi, alifunikwa na kupata nafasi chache na kwenye Kipindi cha Kwanza alionekana akitapika Uwanjani, kitu ambacho humtokea mara kadhaa akicheza Mechi.
Hadi Dakika 90, Mechi hii ilikuwa Sare 0-0.
Dakika chache kabla Mechi kuanza Germany walilazimika kumbadili Kiungo wao Sami Khedira, ambae alipata maumivu ya Musuli ya Mguu wakati akipasha moto mwili, na kumwingiza Christoph Kramer, Mchezaji wa Klabu ya Borussia Monchengladbach.
Lakini nae Kramer alidumu Dakika 32 tu baada ya kuumia alipogongana na Mabeki wa Argentina kabla ya hapo na kushindwa kuendelea baada kusikia kizunguzungu na nafasi yake kuchukuliwa na Mchezaji wa Chelsea, Andre Schurrle.
Kipindi cha Kwanza Germany walitawala na kupata nafasi kadhaa lakini Argentina walionekana hatari wakishambulia kwa kustukiza.
Argentina walipata nafasi safi kwenye Dakika ya 20 wakati Toni Kroos alipofanya makosa kwa kupiga Kichwa cha nyuma kumrudishia Kipa na Mpira kunaswa na Gonzalo Higuaian, ambae akimkabili Kipa wa Germany Manuel Neuer, alipiga fyongo na kutoa Mpira nje.
Lakini Argentina walimudu kufunga Bao kupitia Gonzalo Higuain kwenye Dakika ya 29 na kukataliwa kwa Ofsaidi ambayo ilikuwa ni ya kweli.
Nafasi kubwa kwa Germany ilikuja kabla tu ya Haftaimu wakati Kona ilipounganishwa na Benedikt Howedes kwa Kichwa na Mpira kupiga Posti.
Hadi Mapumziko Bao zilikuwa 0-0.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Argentina kufanya mabadiliko na kumtoa Ezequiel Lavezzi na kumwingiza Sergio Aguero.
Lakini kila Timu iliendelea kukosa nafasi za wazi na nyingi zikiwaangukia Germany huku Toni Kroos akizikosa kadhaa.
Hadi Dakika 90 kwisha, Bao zilibaki 0-0.
Dakika za Nyongeza 30 zikawadia na kwenye Kipindi cha Kwanza cha muda huo, Dakika 15 za kwanza, Bao zilibaki hivyo 0-0 huku kila upande ukiendelea kupata nafasi bila kuzitumia ipasavyo.
Moja ya nafasi hizo ni ile ya Rodrigo Palacio ambapo alimzidi mbio Beki wa Germany, Matt Hummels, na kukabiliana Kipa Neur lakini akautoa Mpira nje.
Kwenye Kipindi cha Pili vuta nikuvute iliendelea na Argentina walibahatika sana pale Sergio Aguero alipompasua chini ya jicho Kiungo wa Germany Schweinsteiger kwa kutumia mkono wake lakini Refa Rizzoli kutoka Italy hakumpa Kadi Nyekundu Muargentina huyo.
Ndipo Dakika ya 113, Mario Gotze, alieingizwa kutoka Benchi kwenye Dakika ya 88 kumbadili Miroslav Klose, kuifungia Bao pekee na la ushindi baada kupokea Krosi safi kutoka kushoto ya Andre Schurrle na kuiweka gambani kabla kuachia Shuti lililompita Kipa Sergio Romero.
Hizi ni fainali za 20 na  ni mara ya pili kwa brazil kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia, mara ya kwanza ilikuwa mwaka 1950
Fainali zijazo za Kombe la Dunia, Mwaka 2018, zitachezwa huko Urusi.
KOMBE LA DUNIA 2014
RATIBA & MATOKEO TANGU MWANZO MAPAKA FAINALI
ALHAMISI, JUNI 12, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Brazil  3 Croatia 1
A
Arena Corinthians
IJUMAA, JUNI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Mexico 1 Cameroon 0
A
Estadio das Dunas
2200
Spain  1 Netherlands 5
B
Arena Fonte Nova
0100
Chile  3 Australia 1
B
Arena Pantanal
JUMAMOSI, JUNI 14, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Colombia 3 Greece 0
C
Estadio Mineirão
2200
Uruguay 1 Costa Rica 3
D
Estadio Castelão
0100
England 1 Italy 2
D
Arena Amazonia
0400
Ivory Coast 2 Japan 1
C
Arena Pernambuco
JUMAPILI, JUNI 15, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Switzerland 2 Ecuador 1
E
Nacional
2200
France 3 Honduras 0
E
Estadio Beira-Rio
0100
Argentina 2 Bosnia-Herzegovina 1
F
Estadio do Maracanã
JUMATATU, JUNI 16, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Germany 4 Portugal 0
G
Arena Fonte Nova
2200
Iran 0 Nigeria 0
F
Arena da Baixada
0100
Ghana 1 United States 2
G
Estadio das Dunas
JUMANNE, JUNI 17, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Belgium 2 Algeria 1
H
Estadio Mineirão
2200
Brazil 0 Mexico 0
A
Estadio Castelão
0100
Russia 1 South Korea 1
H
Arena Pantanal
JUMATANO, JUNI 18, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Australia 2 Netherlands 3
B
Estadio Beira-Rio
2200
Spain 0 Chile 2
B
Estadio do Maracanã
0100
Cameroon 0 Croatia 4
A
Arena Amazonia
ALHAMISI, JUNI 19, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Colombia 2 Ivory Coast 1
C
Nacional
2200
Uruguay 2 England 1
D
Arena Corinthians
0100
Japan 0 Greece 0
C
Estadio das Dunas
IJUMAA, JUNI 20, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Italy 0 Costa Rica 1
D
Arena Pernambuco
2200
Switzerland 2 France 5
E
Arena Fonte Nova
0100
Honduras 1 Ecuador 2
E
Arena da Baixada
JUMAMOSI, JUNI 21, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina 1 Iran 0
F
Estadio Mineirão
2200
Germany 2 Ghana 2
G
Estadio Castelão
0100
Nigeria 1 Bosnia-Herzegovina 0
F
Arena Pantanal
JUMAPILI, JUNI 22, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Belgium 1 Russia 0
H
Estadio do Maracanã
2200
South Korea 2 Algeria 4
H
Estadio Beira-Rio
0100
United States 2 Portugal 2
G
Arena Amazonia
JUMATATU, JUNI 23, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Australia 0 Spain 3
B
Arena da Baixada
1900
Netherlands 2 Chile 0
B
Arena Corinthians
2300
Croatia 1 Mexico 3
A
Arena Pernambuco
2300
Cameroon 1 Brazil 4
A
Nacional
JUMANNE, JUNI 24, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Italy 0 Uruguay 1
D
Estadio das Dunas
1900
Costa Rica 0 England 0
D
Estadio Mineirão
2300
Japan v Colombia
C
Arena Pantanal
2300
Greece v Ivory Coast
C
Estadio Castelão
JUMATANO, JUNI 25, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Nigeria 2 Argentina 3
F
Estadio Beira-Rio
1900
Bosnia-Herzegovina 3 Iran 1
F
Arena Fonte Nova
2300
Honduras 0 Switzerland 3
E
Arena Amazonia
2300
Ecuador 0 France 0
E
Estadio do Maracanã
ALHAMISI, JUNI 26, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
United States 0 Germany 1
G
Arena Pernambuco
1900
Portugal 2 Ghana 1
G
Nacional
2300
South Korea 0 Belgium 1
H
Arena Corinthians
2300
Algeria 1 Russia 1
H
Arena da Baixada
JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Brazil 1 Chile 1 [Penati 3-2] [Mechi Na. 49]
RAUNDI YA PILI
Estadio Mineirão
2300
Colombia 2 Uruguay 0 [50]
RAUNDI YA PILI
Estadio do Maracanã
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Netherlands 2 Mexico 1 [51]
RAUNDI YA PILI
Estadio Castelão
2300
Costa Rica 1 Greece 1 [Penati 5-3] [52]
RAUNDI YA PILI
Arena Pernambuco
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
France 2 Nigeria 0 [53]
RAUNDI YA PILI
Nacional
2300
Germany 0 Algeria 0 [Dakika 120, 2-1] [54]
RAUNDI YA PILI
Estadio Beira-Rio
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina 0 Switzerland 0 [Dak 120, 1-0] [55]
RAUNDI YA PILI
Arena Corinthians
2300
Belgium 0 USA 0 [Dak 120, 2-1] [56]
RAUNDI YA PILI
Arena Fonte Nova
ROBO FAINALI
IJUMAA, JULAI 4, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
France 0 Germany 1 [57]
ROBO FAINALI
Estadio do Maracanã
2300
Brazil 2 Colombia 1 [58]
ROBO FAINALI
Estadio Castelão
JUMAMOSI, JULAI 5, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
1900
Argentina 1 Belgium 0 [59]
ROBO FAINALI
Nacional
2300
Netherlands 0 Costa Rica 0  Penati 4-3] [60]
ROBO FAINALI
Arena Fonte Nova
NUSU FAINALI
JUMANNE, JULAI 8, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Germany 1 Brazil 7 [61]
NUSU FAINALI
Estadio Mineirão
JUMATANO, JULAI 9, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Argentina 0 Nertherlands 0 Penati 4-2] [62]
NUSU FAINALI
Arena Corinthians
MSHINDI WA TATU
JUMAMOSI, JULAI 12, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2300
Brazil 0 Netherlands 3
MSHINDI WA 3
Nacional
FAINALI
JUMAPILI, JULAI 13, 2014
SAA
MECHI
KUNDI
UWANJA
2200
Germany 0 Argentina 0 [Dak 120, 1-0]
FAINALI
Estadio do Maracanã
VIWANJA:
Rio de Janeiro: Maracanã (Viti 71,159) 
São Paulo: Arena de São Paulo (Arena Corinthians – Viti 59,955) 
Belo Horizonte: Mineirão (Viti 56,091)
Brasilia: Estádio Nacional de Brasilia (Viti 65,702)
Fortaleza: Arena Castelão (Viti 57,747)
Salvador: Arena Fonte Nova (Viti 49,280) 
Porto Alegre: Estádio Beira-Rio (Viti 42,153) 
Recife: Arena Pernambuco (Viti 40,604) 
Manaus: Arena da Amazônia (Viti 39,573) 
Cuiabá: Arena Pantanal (Viti 39,553) 
Natal: Arena das Dunas (Viti 39,304) 
Curitiba: Arena da Baixada (Viti 37,634) 
MAKUNDI NDO HAYA
KUNDI A
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Brazil
3
2
1
0
7
2
5
7
Mexico
3
2
1
0
4
1
3
7
Croatia
3
1
0
2
6
6
0
3
Cameroon
3
0
0
3
1
9
-8
0

KUNDI B
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Netherlands
3
3
0
0
10
3
7
9
Chile
3
2
0
1
5
3
2
6
Spain
3
1
0
2
4
7
-3
3
Australia
3
0
0
3
3
9
-6
0

KUNDI C
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Colombia
3
3
0
0
9
2
7
9
Greece
3
1
1
1
2
4
-2
4
Ivory Coast
3
1
0
2
4
5
-1
3
Japan
3
0
1
2
2
6
-4
1

KUNDI D
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Costa Rica
3
2
1
0
4
1
3
7
Uruguay
3
2
0
1
4
4
0
6
Italy
3
1
0
2
2
3
-1
3
England
3
0
1
2
2
3
-1
1

KUNDI E
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
France
3
2
1
0
8
2
6
7
Switzerland
3
2
0
1
7
6
1
6
Ecuador
3
1
0
2
3
3
0
3
Honduras
3
0
0
3
1
8
-7
0
KUNDI F
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Argentina
3
2
0
0
6
3
3
9
Nigeria
3
1
1
1
3
3
0
4
Bosnia
3
1
0
2
4
4
-0
3
Iran
3
0
1
2
1
4
-3
1

KUNDI G
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Germany
3
2
2
0
7
2
5
7
United States
3
1
2
0
4
4
0
4
Portugal
3
1
1
1
4
7
-3
4
Ghana
3
0
1
2
4
6
-2
1

KUNDI H
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
Belgium
2
2
0
0
3
1
2
6
Algeria
2
1
0
1
5
4
1
3
Russia
2
0
1
1
1
2
-1
1
South Korea
2
0
1
1
3
5
-2
1

KWA HERI TUKUTANE FAINALI ZIJAZO 2018  MUNGU AKITUJALIA UZIMA

No comments: