WIVU WA MAPENZI WASABABISHA KIFO HUKO MPANDA
Kamanda polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari |
MWANAMKE mmoja aliyefahamika kuwa
ni Cesilia Clementi (22) Mkazi wa Mtaa wa Majengo B Mjini Mpanda ameuawa
kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu mbalimbali za mwili wake na mpenzi
wake aliyefahamika kwa jina moja la Kanu ambaye ni mfanyabiashara wa
Mpunga wa kutoka mkoani Kigoma.
Kwa mujibu wa
Kamanda polisi mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, tukio hilo la mauaji ya
kusikikisha ya mwanamke huyo limetokea hapo juzi saa mbili asubuhi
nyumbani kwa shemeji ya marehemu aitwaye Mashaka Hanja katika
Mtaa huo wa majengo mjini hapa
Alisema kuwa kabla
ya tukio hilo marehemu ambaye alikuwa akiishi kwa dada yake mke wa Mashaka
Hanja walikuwa wanamahusiano ya kimapenzi na mpangaji wa
nyumba hiyo, ambapo aliamka asubuhi na kuanza kufagia nje ya nyumba hiyo.
Wakati akiwa anaendelea
kufagia ndipo Kanu alitoka ndani na kumwita mpenzi wake huyo na kisha waliingia
ndani ya chumba alichokuwa wakiishi ghafla majirani
walianza kusikia marehemu akishutumiwa na Kanu kuwa siku hizi hamjali kwa
kuwa ameisha pata mwanaume mwingine.
Walieleza
baada ya mabishano ya muda mfupi walisikia marehemu akipiga
mayowe ya kuomba msaada na majirani hao walipojaribu kufungua
mlango walishindwa kwani ulikuwa umefungwa kwa ndani.
Aliongeza kuwa
majirani hao walijaribu kumsihi Kanu afungue mlango lakini hakufanya
hivyo hali ambayo iliwalazimu wachungulie dirishani na
kumwaona Kanu akimchoma marehemu na kisu kwenye sehemu mbalimbali
za mwili wake.
Polisi walipata
taarifa hizo na mara walifika kwenye eneo hilo huku wakiwa na
silaha na kuweza kuvunja mlango na walipoingia ndani walikuta marehemu akiwa
ameishafariki dunia huku mwili wake ukiwa unagalagala chini ya sakafu
Na Kanu akiwa hoi
huku na hana fahamu baada ya kuona amemuua mpenzi wake na yeye kuamua kujichoma
kisu katika sehemu ya tumbo na shingoni
Jeshi la
polisi Mkoa wa Katavi limethibitisha kutokea kwa mauaji ya mwanamke
huyo na wanamshikilia mtuhumiwa huyo huku akiwa amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Mpanda.
No comments:
Post a Comment