Friday, June 27, 2014

PATASHIKA RAUNDI YA MTOANO KOMBE LA DUNIA KUANZA JUMAMOSI

FAINALI za Kombe la Dunia huko Brazil sasa zimeingia Hatua ya Mtoano na zipo Timu 16 zinazowania kutinga Robo Fainali.
Jumamosi, Juni 28, Wenyeji Brazil watacheza na wenzao wa Marekani ya Kusini Chile huko Estadio Mineirao Jijini Belo Horizonte.
Baadae Siku hiyo hiyo, Colombia wataivaa Uruguay Uwanjani Maracana Jijini Rio de Janeiro na Uruguay watacheza bila ya Straika wao Luis Suarez, anaechezea Liverpool huko England baada Mchezaji huyo kupigwa rungu na FIFA na kufungiwa Miezi Minne kutoshiriki shughuli yeyote ya Soka pamoja na Mechi 9 za Uruguay baada kupatikana na hatia ya kumng’ata Meno Beki wa Italy, Giorgio Chiellini.
Mbali ya Timu kuwania kutinga Robo Fainali pia ipo vita binafsi ya kugombea Buti ya Dhahabu na hadi sasa Wachezaji Watatu wanafukuzana wakiwa na Bao 4 kila mmoja.
Hao wanne ni Thomas Muller wa Germany, ambae ndie alietwaa Tuzo hiyo Fainali zilizopita Mwaka 2010 huko Afrika Kusini, Lionel Messi na Supastaa wa Brazil, Neymar.
KOMBE LA DUNIA
RAUNDI YA PILI YA MTOANO
JUMAMOSI, JUNI 28, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
49
Brazil v Chile
Mineirão
Belo Horizonte
2300
50
Colombia v Uruguay
Maracanã
Rio de Janeiro
JUMAPILI, JUNI 29, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
51
Netherlands v Mexico
Castelao
Fortaleza
2300
52
Costa Rica v Greece
Pernambuco
Recife
JUMATATU, JUNI 30, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
53
France v Nigeria
Nacional
Brasilia
2300
54
Germany v Algeria
Beira-Rio
Porto Alegre
JUMANNE, JULAI 1, 2014
SAA
MECHI NA
MECHI
UWANJA
MJI
1900
55
Argentina v Switzerland
Corinthians
Sao Paulo
2300
56
Belgium v USA
Fonte Nova
Salvador







No comments: