KUELEKEA BRAZIL FIFA INA
IMANI NA MICHUANO YA MWAKA HUU
Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa
amesema kuwa ana imani kuwa kombe la dunia nchini Brazil litakuwa na ufanisi
mkubwa.
Bwana Sepp Blatter ametoa wito kwa raia wa
Brasil wajitolee vilivyo kusaidia kufanikisha mchezo huo mwaka huu.
Matamshi ya Bwana Blatter yamekuja huku hofu
ikielezewa mjini Sao Paulo juu ya msongamano mkubwa wa watu na magari kufuatia
mgomo wa wafanyikazi wa shirika la reli.
Maafisa wakuu wa Fifa wenyewe walikwama
katika foleni ndefu ya magari barabarani.
Usafiri huo unatarjaiwa kutatizika zaidi
kufatia kuvunjika kwa mazungumzo kati ya muungano wa wafanyikazi hao na serikali.
Orodha kamilifu ya timu zitakazoshiriki
michuano wa Kombe la Dunia imetolewa. Majina ya makocha 32 ambao watasimamia
mechi za mashindano hayo, pia majina ya wachezaji 736 watakaoshiriki mechi hizo
zitakazochezwa kati ya Juni 12 hadi Julai 13 zimetangazwa..
Taarifa zaidi iliyotolewa ni kuwa timu
zimepunguza idadi ya wachezaji, majeraha kukaguliwa na hali ya afya ya
wachezaji kutathminiwa. Haya yote yakiwa ni matayarisho kwa michuano hayo
yatakayo anza jijini Sao Paulo.
Timu zote zimetayarisha wachezaji 23 ambao
kwa sasa watazingatia uwezo wa kufanikisha timu zao.
No comments:
Post a Comment