POLISI
WA SKETI FUPI AENDA MAHAKAMANI KUOKOA KAZI YAKE
Koplo
wa Kitengo cha Traffiki aliyepigwa picha akiwa amevalia sketi iliyomabana
makalio amelazimika kukimbilia mahakamani kuokoa kazi yake.
Linda
Okello alikimbilia Mahakamani Baada ya wakubwa wake kutaka kumchukulia hatua ya
kinidhamu wakidai alikosa nidhamu ya kazi alipovalia sketi iliyoonesha umbo
lake akiwa kazini.
Kinyume
na kanuni za idara ya polisi ya mwaka wa 2011.
Dada
huyo aliyezua mjadala kote duniani kuhusu wanawake waliojaliwa makalio makubwa
na kama wanabaguliwa kutokana na maumbile yao amemshtaki Inspekta mkuu wa
polisi nchini Kenya miongoni mwa tume inayosimamia polisi nchini humo.
Koplo
Linda anasema kuwa Afisa mkuu wa wilaya ya kiambu Stephen Ngetich hata hakuwepo
katika eneo la tukio lakini ndiye aliyemshmtaki.
Linda
alipigwa picha akilinda usalama katika mashindano ya mbio za magari ya Kiambu
na picha hiyo ikaenea sana katika mitandao ya kijamii kuhusiano na urefu wake
na pia makalio na umbo lake .
Sasa
koplo huyo anaitaka mahakama ifutilie mbali kesi ilyoko dhidi yake akisema,kuwa
anahisi ataonewa na wakubwa wake kutokana na majaliwa yake .
Aidha
koplo huyo huyo anasema kuwa japo alipewa Suruali ndefu mbili iliasiivae tena
sketi hiyo yake, Koplo huyo anadai kuwa bosi wake hakuwahi kumkaripia kwa
kuivalia na kuwa madai dhidi yake yanashinikizwa tu na watu waliovutiwa na
mjadala katika mitandao ya kijamii.
Alipigwa
picha na mwanahabari mmoja wa gazeti moja maarufu nchini Kenya akiwa na wenzake
kazini mjini Kiambu.
Lakini
punde si punde picha hiyo ikaanza kusambazwa kwa mitandano ya kijamii na baadhi
wakiikejeli.
Taarifa
ya polisi huyo kuonywa ilizua hasira kwenye mitandao ya kijamii baadhi wakihoji
ikiwa ni makosa kwa afisaa wa polisi kuvalia sketi ya kumbana.
BBC
No comments:
Post a Comment