MAJARIBIO YA UWANJA WA SAO PAULO
NCHINI BRAZIL YAPATA MAFANIKIO MAKUBWA
![]() |
Arena de Sao Paulo |
Uwanja utakaotumika siku ya mechi ya ufunguzi kati ya
waandaaji wa kombe la dunia Brazil na Croatia Juni 12, Arena de Sao Paulo sasa
upo tayari kwa mashindano ambayo yanashughulikiwa na FIFA na kamati ya
maandalizi ya mashindano hayo nchini Brazil LOC.
Uwanja huo ambao ni wa mwisho kujaribiwa ulichezewa
mechi ya kwanza Jumapili kati ya wenyeji Corinthians na Figueirense, ambapo
wageni waliibuka na ushindi wa 1-0.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari
mkurugenzi wa kamati ya maandalizi Ricardo Trade amesema ameridhishwa na
kufurahishwa na namna operesheni ilivyokwenda.
Akizungumza kwa
niaba ya wenyeji Corinthians baada ya mechi hiyo, Andres Sanchez amesema mechi
hiyo imeipatia uzoefu mpya klabu yake. Kwa upande wake msimamizi maalumu wa
kombe la dunia wa sekretariet ya FIFA huko Sao Paulo Raquel Verdenacci pia
ameeleza kuridhishwa na jinsi mashabiki walivyowasili na kuondoka katika mechi
ya majaribio.
No comments:
Post a Comment