WANAWAKE WALILIA MAHABA YA MAPADRE WATAKA WARUHUSIWE KUOA
![]() |
Papa Francis |
Kundi
moja la wanawake walio na hisia za kimapenzi na mapadre wa kikatoliki
wamemuandikia barua kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis ya kumtaka
kubadilisha sheria za kanisa hilo zinazowazuia viongozi hao wa dini kuoa.
Wanawake
hao 26 kutoka Italy na maeneo mengine wanasema kwamba wamekuwa wakishiriki ama
wanataka kushiriki katika uhusiano wa kimapenzi na mapadre na kwamba wametoa
ombi hilo kwa niaba ya wanawake wengine ambao wako katika hali kama hiyo.Barua hiyo inazungumzia kuhusu uchungu wa kushindwa kuishi maisha yao kikamilifu mbali na kutaka kukutana na papa Francis.
Papa Francis amekuwa akiunga mkono utamaduni wa useja,lakini mwaka 2010 aliandika akisema kuwa huenda msimamo wake ukabadilika.
Papa francis amekuwa akimtembelea mjane wa aliyekuwa kasisi Jeronimo Podesta ambaye alijiuzulu katika utumishi wake na kuoa, zaidi ya miaka 40 iliopita.
BBC
No comments:
Post a Comment