TANZANIA
U-15 YAKAMATA NAFASI YA PILI AFRIKA AYG
![]() |
Afisa habari wa TFF Bonifas Wambura |
Tanzania imeshika nafasi ya pili kwenye Michezo ya Afrika
kwa Vijana (AYG) kwa upande wa mpira wa miguu kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 15 baada ya jana (Mei 29 mwaka huu) kuilaza Afrika Kusini mabao 2-0.
Mechi hiyo ilichezwa Uwanja wa SSKB jijini Gaborone
ambapo kwa matokeo hayo Tanzania imetwaa medali ya fedha baada ya kushika
nafasi ya pili. Nigeria ndiyo ilishika nafasi ya kwanza na kutwaa medali ya
dhahabu.
Tanzania imemaliza ikiwa na pointi kumi ambapo ilishinda
mechi tatu, sare moja na kupoteza moja mbele ya Nigeria.
Katika mechi ya kwanza ilitoka sare ya bao 1-1,
ikawafunga Botswana 2-0, Swaziland wakachapwa 3-0 na baadaye kuwafunga Afrika Kusini
2-0. Timu ya Tanzania inayofundishwa na kocha Abel Mtweve ilifungwa na Nigeria
mabao 2-0.
Wachezaji 16 waliounda kikosi hicho cha Tanzania katika
michezo hiyo inayomalizika leo (Mei 30 mwaka huu) ni Adam Shayo, Amani Ally,
Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove
Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo
Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.
Nchi nyingine zinazoshiriki michezo hiyo kwa upande wa
mpira wa miguu ni Afrika Kusini, Botswana, Nigeria, Mali na Swaziland wakati
Gabon na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) zilijitoa dakika za mwisho
No comments:
Post a Comment