CHAMA cha Soka nchini
Italia kimethibitisha kuwa kiungo wa klabu ya Lazio, Joseph Minala hakudanganya
kuhusiana na umri wake. Mtandao mmoja wa soka barani Afrika ulitoa madai
Februari mwaka huu kuwa Minala ambaye ni mzaliwa wa Cameroon ana umri wa miaka
42 na sio miaka 17 anayotaja yeye.
Suala hilo lilipelekea
maofisa kufanyia uchunguzi taarifa hizo ambapo ilipelekea Manala mwenye
kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo. Katika taarifa yake mara baada ya
uchunguzi FIGC ilidai kuwa hawakupata ushahidi wowote ambao ungepelekea hatua
za nidhamu kuchukuliwa. Minala alijiunga na Lazio yenye maskani yake
jijini Rome majira ya kiangazi mwaka jana na aliiwakilisha timu hiyo katika
michuano ya vijana ya Kombe la Viareggio Februari mwaka huu.
No comments:
Post a Comment