MASHUJAA WA TANZANIA KUWASILI LEO, PONGEZI ZAMIMINIKA.
KIKOSI cha Taifa Stars ambacho jana (Juni 1 mwaka huu)
kiliitupa Zimbabwe (Mighty Warriors) nje ya michuano ya Afrika baada ya kutoka
sare ya mabao 2-2 kinarejea nchini leo (Juni 2 mwaka huu) kutoka
Harare. Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itatua
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) jijini Dar es Salaam saa
12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Harare kupitia
Nairobi. Stars imefuzu kucheza raundi inayofuata kwa ushindi wa jumla ya
mabao 3-2, kwani awali (Mei 18 mwaka huu) iliifunga Zimbabwe bao 1-0 katika
mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika raundi
ya pili, Taifa Stars itacheza na Msumbiji ambapo itaanzia nyumbani kati ya
Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya
Agosti 2 na 3 mwaka huu. Wakati huo huo, Taifa Stars imeendelea kupokea
salamu za pongezi kutoka kwa wadau mbalimbali baada ya kufanikiwa kuvuka
kikwazo hicho cha kwanza katika harakati zake za kucheza Fainali za Afrika
zitakazofanyika mwakani nchini Morocco. Salamu hizo zimetoka kwa Chama cha
Mpira wa Miguu Mkoa wa Mbeya (MREFA), Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Manyara
(MARFA), mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
akiwakilisha Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mwanza (MZFA), John Kadutu, na
mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Ahmed Idd Mgoyi.
U15 TANZANIA YATUA MEDALI VIFUANI
TIMU ya Tanzania ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 15 iliyoshika nafasi ya pili katika Michezo ya Afrika kwa Vijana (AYG) iliyofanyika Gaborone, Botswana inawasili leo (Juni 2 mwaka huu) jijini Dar es Salaam. U15 ambayo imeshinda mechi tatu, sare moja na kufungwa moja inawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 12.30 jioni kwa ndege ya Kenya Airways ikitokea Gaborone kupitia Nairobi. Tanzania ambayo imepata medali za fedha kwa kushika nafasi hiyo ikiwa chini yaKocha Abel Mtweve ilizifunga Afrika Kusini 2-0, Botswana 2-0, Swaziland 3-0 na ikatoka sare ya bao 1-1 na Mali. Ilifungwa mabao 2-0 na Nigeria ambao ndiyo walioibuka mabingwa. Wachezaji 16 waliounda kikosi cha Tanzania ni Adam Shayo, Amani Ally, Amos Manguli, Amri Nyuki, Amede Amani, Baraka Rashid, David Uromi, Goodlove Mdumule, Hance Msonga, Kelvin Kamalamo, Makalius Amrin, Nasson Chanuka, Paulo Ngowi, Petro Shaban, Rajab Mohamed na Thomas Chindeka.

No comments:
Post a Comment