TAARIFA KUTOKA TFF LEO
WACHEZAJI 31 wameteuliwa kujiunga na timu
ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili
ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini
Senegal. Ngorongoro Heroes itakayokuwa chini ya Kaimu Kocha John Simkoko
akisaidiwa na Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho (Machi 19 mwaka huu) jijini
Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayochezwa kati
ya Aprili 4-6 jijini Nairobi. Kikosi kinachounda timu hiyo ambayo
itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Dar es Salaam
kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa
vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars. Wachezaji walioitwa ni
makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter
Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende,
Zanzibar). Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward
Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel
Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed
(Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki
Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji). Viungo ni Ally
Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid
Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim
(Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma (Acudu,
Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma
(Scouting- Ruvuma) na Tumaini John (Scouting- Mwanza). Washambuliaji ni
Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar),
Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT),
Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).
MICHUANO ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho
(Machi 19 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Azam itakayochezwa Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni. Tiketi kwa ajili ya mechi
hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu kwenye vituo vya Shule
ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa
Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha
daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa. Baada ya saa 6 mchana mauzo yote
yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi
kuanzia saa 7.30 mchana. Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000
kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na
kijani kiingilio ni sh. 7,000. Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Hashim
Abdallah wa Dar es Salaam ambapo atasaidiwa na Anold Bugado (Singida),
Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam). Kamishna wa mechi
hiyo Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza
wa Mwanza.
No comments:
Post a Comment