Thursday, March 13, 2014

TANZANIA YASHUKA NAFASI 1 LISTI YA UBORA DUNIANI YA FIFA
LISTI YA UBORA DUNIANI iliyotolewa Leo na FIFA imebaki vile vile kwa Timu za Juu kwa Mabingwa wa Dunia, Spain, kuendelea kukamata Nambari Wani na Timu ya Juu kabisa kwa Afrika ni Ivory Coast, iliyoporomoka Nafasi 1 na kukaa Nafasi ya 24 huku nayo Tanzania ikishuka Nafasi moja na kushika Nafasi ya 117.
Timu za 1 hadi 5 zimebaki pale pale na Uruguay kupanda Nafasi 1 na kushika Nafasi ya 6, Uswisi kushuka moja na wako Namba 7, Italy na Brazil kubaki Namba zao za 8 na 9 huku Belgium wakiingia 10 Bora na kushika Nafasi ya 10 kwa kuitoa Netherlands ambayo sasa iko Nafasi ya 11.

Listi nyingine ya Ubora Duniani itatolewa hapo Aprili 10.

JIRANI ZA TANZANIA:

115    Mozambique

116    Lebanon

117    Tanzania

118    New Caledonia

119    Equatorial Guinea

120    Luxembourg

No comments: