Wednesday, March 19, 2014

CHELSEA NA REAL ZAINGIA ROBO FAINALI UEFA CHAMPIONZ LIGI

CHELSEA 2 GALATASARAY 0
Bao za Samuel Eto'o, Dakika ya 4, na Gary Cahill, Dakika ya 43, zimeifanya Chelsea itinge Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ LIGI baada ya kuichapa Galatasaray Bao 2-0 Uwanjani Stamford Bridge.
Katika Mechi ya Kwanza huko Ugiriki, Timu hizi zilitoka 1-1.
REAL MADRID 3 SCHALKE 1
Bao mbili za Cristiano Ronaldo, Dakika ya 22 na 74, na moja la Morata, Dakika ya 75, zimewapa ushindi Real Madrid wa Bao 3-1 na kuwabwaga nje ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Schalke kwa Jumla ya Mabao 9-2 katika Mechi mbili.
Bao pekee la Schalke kwenye Mechi hii lilifungwa na Tim Hoogland katika Dakika ya 31.
TIMU ZILIZOTINGA ROBO FAINALI:
Bayern Munich
Atletico Madrid
Barcelona
Paris Saint-Germain
Chelsea
Real Madrid

MECHI ZA LEO JUMATANO MACHI 19

22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg

22:45 Manchester United v Olympiacos CFP

No comments: