BARCA,
PSG ZAUNGANA NA BAYERN & ATLETICO ROBO FAINALI

Kipindi cha Pili, Dakika ya 67, Lionel Messi alifunga Bao kwa Barca baada ya Difensi ya City kujichanganya.
Kwenye Dakika ya 67, City walibaki Mtu 10 pale Zabaleta alipopewa Kadi ya Njano ya Pili alipolalamika kwa Refa kunyimwa kwao Penati wakati Pique alipomkabili Dzeko ndani ya Boksi.
City walisawazisha katika Dakika ya 89 kupitia Nahodha wao Vincent Kompany lakini Barca wakapiga Bao la Pili katika Dakika za Majeruhi baada Andres Iniesta kutumbia kwenye Boksi, kumhadaa Kipa Joe Hart na kumpasia Dani Alves aliewasha kigongo.
Barca wametinga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 4-1.
PARIS ST-GERMAIN 2- 1 BAYER LEVERKUSEN
Bayer Leverkusen walitangulia kupata Bao katika Dakika ya 6 kupitia Sidney Sam na PSG kusawazisha kwa Bao la Marquinhos Dakika 7 baadae.
Lakini Leverkusen wangeweza kufunga Bao la Pili katika Kipindi cha Kwanza walipopata Penati kufuatia rafu ya Jallet kwa Derdiyok ambayo Kipa wa PSG, Sirigu, aliokoa vizuri Penati hiyo iliyopigwa na Rolfes.
Dakika ya 54, Lavezzi aliipa PSG Bao la Pili na kufanya Gemu iwe 2-1 na PSG kusonga Robo Fainali kwa Jumla ya Bao 6-1
No comments:
Post a Comment