TAARIFA KUTOKA TFF LEO
22 KUSHIRIKI SEMINA YA WAAMUZI DAR
Waamuzi
na waamuzi wasaidizi 22 wameteuliwa kushiriki semina na mtihani wa utimamu wa
mwili kwa robo ya kwanza ya mwaka huu itakayofanyika jijini Dar es Salaam
kuanzia Machi 14 hadi 16.
Semina
hiyo inashirikisha waamuzi wote wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA) na wale wa ngazi ya juu (elite) kutoka Tanzania Bara za
Zanzibar.
Waamuzi
hao ni Charles Simon (Dodoma), Dalila Jafari (Zanzibar), Ferdinand Chacha
(Mwanza), Hamis Chang’walu (Dar es Salaam), Helen Mduma (Dar es Salaam), Israel
Mujuni (Dar es Salaam), Issa Vuai (Zanzibar), Janeth Balama (Iringa), Jesse
Erasmo (Morogoro), John Kanyenye (Mbeya) na Jonesia Rukyaa (Bukoba).
Josephat
Bulali (Zanzibar), Lulu Mushi (Dar es Salaam), Martin Saanya (Morogoro), Mfaume
Nassoro (Zanzibar), Mohamed Mkono (Tanga), Mwanahija Makame (Zanzibar), Ngaza
Kinduli (Zanzibar), Oden Mbaga (Dar es Salaam), Ramadhan Ibada (Zanzibar),
Samwel Mpenzu (Arusha) na Waziri Sheha (Zanzibar).
Wakufunzi
wa semina hiyo ambao wanatambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF)
ni Joan Minja na Riziki Majala.
RATIBA VPL YAREKEBISHWA, LIGI KUMALIZIKA APRILI 19
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) ambapo sasa itamalizika Aprili 19 mwaka huu badala ya Aprili 27 mwaka
huu.
Marekebisho
hayo yamefanyika ili kutoa fursa kwa timu ya Taifa (Taifa Stars) kujiandaa kwa
mechi za mchujo la Kombe la Afrika 2015 ambapo itacheza raundi ya awali Mei
mwaka huu.
Kutokana
na marekebisho hayo, Yanga itacheza na Prisons (Uwanja wa Taifa) Machi 26 mwaka
huu katika mechi ya raundi ya 17 wakati Machi 19 mwaka huu kwenye uwanja huo
huo ni Yanga na Azam.
Machi
15 mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Azam na Coastal (Azam Complex), na Mtibwa
Sugar itacheza na Yanga (Jamhuri). Mgambo na Azam zitacheza Machi 26 mwaka huu
Mkwakwani, na Aprili 9 mwaka huu Yanga itaialika Kagera Sugar (Taifa).
Raundi
ya 22 itaanza Machi 22 mwaka huu kwa mechi kati ya Kagera vs Prisons (Kaitaba),
JKT Ruvu vs Mbeya City (Azam Complex), na Rhino vs Yanga (Ali Hassan Mwinyi).
Machi 23 mwaka huu ni Simba vs Coastal (Taifa), Mgambo vs Mtibwa (Mkwakwani),
Ruvu Shooting vs Ashanti (Mabatini) na Azam vs Oljoro (Azam Complex).
Machi
29 mwaka huu itaanza raundi ya 23 kwa mechi kati ya Ashanti vs Oljoro (Azam
Complex) wakati Machi 30 ni Mbeya City vs Prisons (Sokoine), Kagera vs Ruvu
Shooting (Kaitaba), Mtibwa vs Coastal (Manungu), JKT Ruvu vs Rhino (Azam
Complex), Azam vs Simba (Taifa), na Mgambo vs Yanga (Mkwakwani).
Raundi
ya 24 inaanza Aprili 5 mwaka huu kwa Kagera vs Simba (Kaitaba), Ashanti vs
Mbeya City (Azam Complex). Aprili 6 mwaka huu ni Coastal vs Mgambo (Mkwakwani),
Oljoro vs Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), Rhino vs Mtibwa (Ali Hassan Mwinyi),
Ruvu Shooting vs Azam (Mabatini) na Yanga vs JKT Ruvu (Taifa).
Aprili
12 mwaka huu inaanza raundi ya 25 kwa Mtibwa vs Ruvu Shooting (Mabatini),
Coastal vs JKT Ruvu (Mkwakwani), Prisons vs Rhino (Sokoine). Aprili 13 mwaka
huu ni Mgambo vs Kagera (Mkwakwani), Simba vs Ashanti (Taifa), Mbeya City vs
Azam (Sokoine) na Oljoro vs Yanga (Sheikh Kaluta Amri Abeid).
Raundi
ya 26 ni Aprili 19 mwaka huu kwa Rhino vs Ruvu Shooting (Ali Hassan Mwinyi),
Mbeya City vs Mgambo (Sokoine), Prisons vs Ashanti (Jamhuri, Morogoro), JKT
Ruvu vs Azam (Azam Complex), Oljoro vs Mtibwa (Sheikh Kaluta Amri Abeid),
Coastal vs Kagera (Mkwakwani) na Yanga vs Simba (Taifa).
MTIHANI WA MAWAKALA WA WACHEZAJI APRILI 3
Mtihani
kwa ajili ya watu wanaotaka kuwa mawakala wa wachezaji wanaotambuliwa na
Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) utafanyika Aprili 3 mwaka huu
saa 4 kamili asubuhi ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (FIFA).
Kwa
wanaotaka uwakala huo wanatakiwa kujisajili ambapo watapewa kanuni mbalimbali
za FIFA na TFF ili waweze kujiandaa kikamilifu kwa mtihani huo utakaokuwa na
sehemu mbili. Sehemu ya kwanza ya mtihani huo ni maswali kutoka FIFA wakati
nyingine ni kutoka TFF.
Tanzania
ina mawakala watatu tu wa wachezaji wanaotambuliwa na FIFA. Mawakala hao ni Ally
Saleh, John Ndumbaro na Mehdi Remtulla.
No comments:
Post a Comment