MCHUNGAJI AFUMANIWA NA MKEWE, MKE
AMSEMEHE ASEMA YEYE NI KAMA MJESHI ALIYEJERUHIWA
Mchungaji mmoja aliyefumaniwa
akiwa na mke wa mtu hotelini mjini Embu amesamehewa na mke na watoto wake.
Mkewe alisema yeye ni kama mwanajeshi aliyejeruhiwa, na hawawezi kumtoroka
mumewe.
Mchungaji
huyo ameomba msamaha kwa kanisa lake na familia yake kwa yale aliyoyatenda.
Antony
Maina wa kanisa la Kenya Assemblies of God (KAG) ambaye alikuwa ameandamana na
familia yake alisema hakushiriki ngono na mwanamke waliopatikana pamoja katika
hoteli moja mjini Karatina, Nyeri.
“Nataka
kufafanua kuwa siko hapa kujitetea kwa yale yaliotokea. Niko hapa kujulisha
kila mtu nchini kuwa nilifanya makosa na mtu yule nimemkosea sana Mungu
na tayari nishamuomba msamaha. Wanahabari walinisadia sana kwa sababu
ningetenda dhambi nyingi zaidi. Kuja kwenu kulizuia kufanyika kwa mambo mabaya
zaidi,” alisema Kasisi Maina.
Mkewe
Beth Maina alisema familia imemsamehe na watasimama na yeye wakati huu anapokabiliwa
na shutuma hizo.
“Bwanangu
ni kama mwanajeshi aliyejeruhiwa katika makabiliano, wakati mwanajeshi
anapopata majeraha wanajeshi wengine humsaidia bila kumuacha nyuma. Kanisa
linapaswa kumsaidia pia katika suala hili,” alisema Bi Maina.
Kasisi
Maina ambaye pia alikuwa ameandamana na wanawe wawili aliyesema shughuli za
kanisa hilo zitaendelea tu kama kawaida.
Makasisi
wa kanisa hilo walisema Bw Maina kwa sasa amesimamishwa kazi huku uchunguzi
ukiendelea kulingana na kanuni na mafunzo ya dhehebu hilo.
Credit Swahili hub
No comments:
Post a Comment