SHABIKI WA ARSENAL AUA WA
LIVERPOOL WAKITAZAMA MECHI NCHINI KENYA

Marehemu
alikuwa akitazama mchuano kati ya timu ya Arsenal na Liverpool wakati
walipoanza vita katika baa ya Marete eneo la Makutano.
Akithibitisha
kisa hicho, Mkuu wa Polisi eneo hilo Tom Odero alisema mshukiwa David Mwangi,
ambaye ni shabiki wa timu ya Arsenal alimdunga kisu Anthony Muteithia,
shabiki wa Liverpool. Bw Odero alisema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 25
alikufa alipokuwa akipata matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Meru.
“Mshukiwa
alilazimika kutoroka lakini wakazi walifanikiwa kupata pikipiki aliyokuwa nayo
na kuiwasilisha kwa maafisa wa polisi katika kituo cha polisi cha Meru. Msako
wa kumkamata umeanzishwa,”alisema Bw Odero.
Mkuu
huyo wa polisi alisema uchunguzi umeanzishwa kutambua chanzo cha mzozo wa
wawili hao.
Katika
mchezo huo Arsenal walichapwa 5-1 na Liverpool.
Credit Swahili hub
No comments:
Post a Comment