Thursday, February 20, 2014

FAZ NA KLABU ZA ZAMBIA ZAPIGWA RUNGU NA FIFA

KAMATI ya NIDHAMU ya FIFA imekiadhibu Chama cha Soka cha Zambia, FAZ [Football Association of Zambia] pamoja na Klabu zake Wanachama, Zanaco FC, Power Dynamos FC na National Assembly FC, kwa kukiuka taratibu za Uhamisho wa Kimataifa wa Wachezaji.
FAZ imepigwa Faini na FIFA Dola 56,300 kwa kuhamisha Wachezaji 8, Watatu wakiwa wa Kulipwa na Watano Wachezaji wa Ridhaa, bila Hati ya Kimataifa ya Uhamisho, ITC [International Transfer Certificate] na nje ya Kipindi cha Uhamisho rasmi.
Pia FIFA imedai FAZ iliwahamisha hao Wachezaji Watatu wa Kulipwa nje ya Mfumo wao rasmi wa Uhamisho, ITMS, [TMS International Transfer Matching System], ambao ni lazima kwa Wachezaji wa Kulipwa kwa Uhamisho wa Kimataifa.
Kwa upande wa Klabu za Zambia zilizotwangwa Rungu la FIFA ni Zanaco FC waliopigwa Faini Dola 22600 kwa kumhamisha Mchezaji mmoja wa kulipwa bila ITC na nje ya ITMS.
Nazo, Power Dynamos FC na National Assembly FC, zimepigwa Faini Dola 28200 kwa kuhamisha Mchezaji wa Ridhaa bila ITC na nje ya Kipindi cha Uhamisho.
Mfumo wa Mtandaoni wa ITMS ulianza kuwa ni lazima tangu Oktoba 2010.

No comments: