Thursday, February 20, 2014

LIGI YA MABINGWA WENYEJI WAZIDI KUTESWA BAYERN YAIPIGA 2-0 ARSENAL EMIRATES, AC MILAN YABANJULIWA 1-0 SAN SIRO NA ATLETICO
Mabingwa Watetezi Bayern Munich wamefanikiwa kuichapa Arsenal waliokuwa kwao Emirates Bao 2-0 katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Dakika ya 8 Mesut Ozil aliangushwa na Boateng na Penati kutolewa lakini Penati hiyo iliyopigwa hafifu na Ozil iliokolewa na Kipa Manuel Neuer ambae ni Rafiki wa Ozil tangu utotoni.
Kwa Ozil hiyo ni Penati yake ya Tatu mfululizo kukosa akichezea Klabu, nyingine zikiwa Arsenal ilipocheza na Marseille kwenye Makundi ya UCL Msimu huu na kabla wakati akiwa na Real Madrid.
Kwa kawaida Wapiga Penati wa Arsenal ni Olivier Giroud na Mikel Arteta na wote hawakuwamo kwenye Mechi hii.
Kwenye Dakika ya 37 Toni Kroos alipenyeza pasi ya juu kwa Arjen Robben ambae alichomoka na kuipita Difensi na kukontroli Mpira akimhadaa Kipa Wojciech Szczesny ambae alimwangusha na Refa Nicola Rizzoli toka Italy kutoa Penati na Kadi Nyekundu kwa Szczesny.
Lakini David Alaba alikosa Penati hiyo iliyopiga Posti chini na kutoka huku Kipa wa Akiba, Fabianski, alieingizwa baada kutolewa Santi Cazorla ili kukaa langoni ‘akienda mbovu’.
Katika Dakika ya 54, baada kupokea pasi safi toka kwa Nahodha Philip Lahm, Toni Kroos aliachia shuti toka Mita 20 ambalo lilipita juu kulia na kutinga wavuni na kuwapa Byern Munich Bao safi.
Bayern katika Dakika ya 88 baada ya pasi yake kuunganishwa kwa kichwa kilichodunda chini cha Thomas Muller, alieingia Kipindi cha Pili, na kumhadaa Kipa Fabianski.
Kwa ushindi huu wa Bao 2-0, Mabingwa wa Ulaya Bayern Munich wamejiweka katika hali njema kucheza Robo Fainali na Arsenal wanahitaji kushinda 3-0 huko Munich ili wapindue kipigo.
Timu hizi zitarudiana huko Allianz Arena Jijini Munich, Germany hapo Machi 11
AC MILAN 0 ATLETICO MADRID 1
Bao la Dakika ya 82 kwa kichwa cha Straika hatari Diego Costa limewapa Atletico Madrid ushindi wa Bao 1-0walipocheza Ugenini huko San Siro na AC Milan katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Timu hizi zitarudiana huko Estadio Vicente Calderon hapo Machi 11.

No comments: