KENYA
KUNANI: MCHUNGAJI AFIA CHUMBANI KWA MPENZI WAKE AKITOA HUDUMA ZA KIROHO
Kasisi
huyo mwenye umri wa miaka 70 anasemekana kutembelea mwanamke huyo katika mtaa
wa Buruburu Phase 1 mwendo wa saa tano asubuhi na kukaa ndani ya chumba hicho
siku nzima.
Maafisa
wa polisi walisema mwili wa kasisi Geoffrey Maingi ulipatikana bila majeraha
yoyote.
Mkuu
wa Polisi wa Buruburu Richard Kerich alisema kasisi huyo anayehudumu katika
kanisa la Redeemed Gospel Buruburu aliliegesha gari lake katika duka la Tuskys
mtaani humo kabla ya kuelekea kwa mwanamke huyo.
Mwanamke
mwenye chumba hicho alisema kasisi huyo alikuwa ameenda kumuombea na kuongeza
kuwa hakujua iwapo alikuwa mgonjwa.
“Si
mara ya kwanza kwake kuja tushiriki maombi pamoja. Amekuwa akinitembelea mara
kwa mara,” alisema mwanamke huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
Mwanamke
huyo mwenye umri wa miaka 40 aliwaambia polisi kuwa kasisi huyo alianguka
ghafla na kufariki.
Jirani
wa mwanamke huyo alithibitisha kuwa kasisi huyo amekuwa na ziara kadhaa
chumbani humo.
Tukio
hilo lilivutia umati mkubwa huku baadhi ya wakazi wa mtaa huo wakidokeza kuwa
huenda kifo cha pasta huyo kilitokana na matumizi ya dawa za kuongeza ashiki za
mapenzi.
“Hii
ilikuwa adhabu ya Mungu kwa kasisi huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na
mwanamke huyo. Mungu alikuwa anataka kuleta vitendo vyake vya gizani
hadharani,” jirani mmoja alinukuliwa.
Majirani
walisema mwanamke mshukiwa alikosana na mumuwe mwaka uliyopita kufuatia mzozo
wa kifamilia.
Waendesha
teksi walisema kuwa mwanamke huyo aliwaomba msaada ampeleke hospitalini lakini
tayari alikuwa amekufa.
“Alikuja hapa akitaka tumpeleke marehemu
hospitalini lakini baada ya kufika kwake tulipata mwili wake ukiwa baridi
kumaanisha alikuwa ashakufa,” alisema mhudumu wa teksi ambaye alisema baadaye
waliwajulisha maafisa wa polisi.
Polisi
walimzuilia mwanamke huyo kwa saa kadhaa ili kutoa habari kuhusu kisa hicho
lakini wakamwachilia baadaye.
“Tutabaini
chanzo cha kifo cha kasisi baada ya mwili wake kufanyiwa upasuaji, kwa sasa
hauwezi kutoa taarifa yoyote,” alisema Bw Kerich .
Bw
Kerich alisema kuwa polisi wamekusanya bidhaa katika chumba hicho ambazo
zitatumiwa katika uchunguzi.
Mwili
wa marehemu ambao polisi walisema haukuwa na majeraha yoyote ulipelekwa katika
chumba cha kuhifadhia maiti cha City kufanyiwa upasuaji.
Waumini
wa kanisa la Redeemed Gospel Buruburu walifika katika eneo hilo na kuondoa gari
la pasta huyo ili kuzuia wanahabari kulipiga picha.
Swahili hub:
No comments:
Post a Comment