MSEVEN ASAINI MSWADA WA
KUPINGA MAPENZI YA JINSI MOJA

Rais Museveni alitia saini mswada huo
nyumbani kwake katika hafla iliyoshuhudiwa na maafisa wakuu wa serikali pamoja
na wandishi wa habari.
Mswada huo ambao sasa utakuwa sheria, unatoa
adhabu ya kifungo cha miaka 14 jela kwa wale watakaopatikana na hatia kwa mara
ya kwanza,
Adhabu ya maisha jela itatolea kwa watu
watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja zaidi ya mara moja
kati ya watu wawili waliokubaliana kufanya hivyo.
Adhabu hiyo pia itatolewa kwa wale
wanaopatikana na hatia ya kuwahusisha watoto katika vitendo hivyo, walemavu au
kumuambikiza mtu virusi vya Ukimwi.
Mswada huo umepigiwa debe sana nchini Uganda,
lakini mashirika ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu yameulaani.
No comments:
Post a Comment