UEFA CHAMPIONZ LIGI UCL: BARCA
YAIPIGA CITY 2-0 ETIHAD, PSG YAINYUKA 4-0 LEVERKUSEN
UEFA CHAMPIONZ LIGI, imeendelea usiku wa kuamkia leo kwa Timu za Nyumbani zote kutandikwa wakati Barcelonawalipoiwasha Manchester City 2-0 huko Etihad na Paris Saint-Germain kuitandika Bayer Leverkusen Bao 4-0 huko Bay Arena, Jijini Leverkusen, Ujerumani, hizo zikiwa Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
MANCHESTER CITY 0 BARCELONA 2
PENATI
ya Dakika ya 54 ya Lionel Messi iliwafungulia njia Barcelona na kupata ushindi
wa Bao 2-0 walipocheza na Manchester City Uwanjani Etihad katika Mechi ya
Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Penati
hiyo ilitolewa baada ya Demichelis kumwangusha Messi aliekuwa anaenda kukutana
na Kipa Joe Hart na pia kusababisha Beki huyo wa Man City kupewa Kadi Nyekundu
na Refa Jonas Eriksson kutoka Sweden.
Barcelona
walifunga Bao lao la Pili katika Dakika ya 90 kupitia Dani Alves baada ya kazi
nzuri ya Neymar alieingia Kipindi cha Pili.
Timu
hizi zitarudiana huko Nou Camp hapo Machi 12 na City watahitaji kushinda Bao
3-0 ili wasonge Robo Fainali.
BAYER LEVERKUSEN 0 PARIS SAINT-GERMAIN 4
Wakicheza
kwao BayArena Jijini Lerkusen, Nchini Germany, Bayer Leverkusen wametandikwa
Bao 4-0 na Paris Saint-Germain ambao hadi Mapumziko walikuwa mbele kwa Bao 3-0.
Bao
za PSG zilifungwa na Blaise Matuidi, Dakika ya 3, na mbili za Zlatan
Ibrahimovic, kwenye Dakika ya 39 kwa Penati na jingine kwa mzinga mkali nje ya
Boksi katika Dakika ya 42 huku Bao la 4 likipachikwa na Yohan Cabaye kwenye
Dakika ya 88.
Kuanzia
Dakika ya 59, Leverkusen walicheza Mtu 10 baada ya Emir Spahic kupewa Kadi
Nyekundu kufuatia Kadi za Njano mbili.
Leo Jumatano Februari 19
22:45
AC Milan v Atletico de Madrid
22:45
Arsenal FC v Bayern Munich
No comments:
Post a Comment