Saturday, February 15, 2014

YANGA YAMALIZA KAZI COMORO YASHINDA 5-2
Kwenye Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Awali ya Michuano ya CAF ya CHAMPIONZ LIGI iliyochezwa Leo huko Uwanja wa Sheikh Said Mohamed International, Mitsamihuli, Visiwa vya Comoro, Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga, wameitandika Komorozine de Domoni Bao 5-2 na kutinga Raundi ya Kwanza kwa Jumla ya Bao 12-2.Wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Komorozine de Domoni Bao 7-0.
Katika Mechi ya Leo, Bao za Yanga zilifungwa na Hamis Kiiza, Dakika ya 13, Simon Msuva, Dakika ya 37, na Bao 3 za Mrisho Ngassa, kwenye Dakika za 22, 87 na 90.
Yanga sasa imesonga Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI ambapo watakutana na Mabingwa Watetezi, Al Ahly ya Misri, kati ya Februari 28 na Machi 2 na Marudiano kuchezwa kati ya Machi 7 na 9.
KIKOSI CHA YANGA:
Deogratias Munish "Dida", Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani, Athuman Idd "Chuji", Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Hamis Kizza
Akiba: Barthez, Juma Abdul,Luhende, Rajab, Domayo, Dilunga n Bahanuzi

SIMBA MBEA CITY 1-1
Mechi kati ya wenyeji Mbeya City inmekwisha Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na matokeo 1-1.

Mbeya City ndiyo walianza kufunga katika kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao moja.

Lakini Simba walikianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanikiwa kupata bao kuputia Amissi Tambwe.

No comments: