YALIYOJIRI TFF LEO
SEMINA YA WAAMUZI, MAKAMISHNA JAN 13
Semina ya waamuzi na makamishna wa Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inafanyika Januari
13 na 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ndiye anayetarajiwa kufungua semina hiyo.
Wakati huo huo, Chama cha Mpira wa Miguu
Zanzibar (ZFA) kimemwalika Rais Malinzi kuwa mgeni rasmi kwenye mechi
ya robo fainali ya Kombe la Mapinduzi kati ya Simba na Chuoni
itakayochezwa kesho (Januari 8 mwaka huu) saa 2 usiku Uwanja wa Amaan.
MAKOCHA WA LESENI B WAKABIDHIWA VYETI
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine amekabidhi leseni B kwa makocha
walioshiriki kozi iliyofanyika mjini Zanzibar mwaka jana.
Jamhuri Kihwelo alipokea leseni hiyo
inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwa niaba ya
washiriki wengine tisa waliofuzu mafunzo hayo.
Makocha wengine waliofuzu kozi hiyo
iliyoendeshwa na mkufunzi Bhekisisa Boy Mkhonta kutoka Swaziland ni
Abdulghan Msoma, Hafidh Badru, Nasra Juma Mohamed, Gulam Abdallah
Rashid, Mohamed Ayoub Suleiman, Shaaban Ramadhan, John Simkoko na Hemed
Suleiman Ali.
Hivi sasa Tanzania ina makocha 40 wenye
leseni B za CAF baada ya wengine 31 kufuzu katika mafunzo yaliyofanyika
mapema mwaka juzi jijini Dar es Salaam chini ya mkufunzi Honor Janza
kutoka Zambia.
No comments:
Post a Comment