BABU WA MIKA 91 AFUNGA NDOA NA BIBI WA MIAKA78
![]() |
| Mzee Nkwabi Ngobola Kapimbi na mkewe Maria Mkiwa siku ya ndoa yao |
Mwaka mpya mambo mapya, Katika tukio linaloweza kuitwa kama ndoa ya karne, mzee
mmoja mwenye umri wa miaka 91, Nkwabi Ngobola Kapimbi, wiki iliyopita alifunga
pingu za maisha na mkewe Maria Mkiwa (78) mbele ya mchungaji Thobias Shilole wa
Kanisa la Maombezi huko Kibaha mkoani Pwani
“Nimefurahi kufunga ndoa, tukio hili ni muhimu kwangu,
umri wangu ni miaka 91, nimezaliwa mwaka mmoja na Nyerere, mke wangu ana miaka
78, tulionana kwa mara ya kwanza mwaka 1958, tukio hili limefungua ukurasa mpya
wa maisha yangu, najua Mungu yuko pamoja nasi, nina wajukuu 78 na Vitukuu 24.
“Watu wengi wanauliza tulikuwa wapi siku zote hizi, ni
kwamba nilikuwa simuamini sana mke wangu, tulikuwa tukikorofishana lakini bado
tuliweza kudumu. Mungu ni mwema sana,” alisema.
Alisema hajali kama kuna watu watakuwa wakizungumza wanalojua kuhusu ndoa yao, lakini anachofurahi yeye ni kufunga ndoa na mke wake anayempenda.
Alisema hajali kama kuna watu watakuwa wakizungumza wanalojua kuhusu ndoa yao, lakini anachofurahi yeye ni kufunga ndoa na mke wake anayempenda.
“Mara ya kwanza mke wangu alikuwa anasita, lakini
nilisema lazima tukafunge ndoa kwenye kanisa la Mzee wa Upako ( Antony
Lusekelo), nampongeza mchungaji Thobias Shilole kwa kuwa pamoja nasi na
kukubali kubariki ndoa yetu, lilikuwa jambo la furaha kwangu na mke wangu,”
alisema Babu Nkwabi.
Kwa upande wake, mkewe Maria alisema awali alikuwa
akisita kwa kuona kama itakuwa ni kituko mbele ya jamii, lakini baada ya
majadiliano na mumewe, akaridhia jambo hilo kwa moyo mmoja.
“Najua maneno lazima yasemwe lakini mimi nampenda sana
mpenzi wangu, tuliwahi kupitia mambo magumu, milima na mabonde lakini leo
tumeamua kuzishinda hila za muovu ya shetani, si kitu cha kawaida kufunga ndoa
kwa umri wetu lakini Mungu ndiyo njia ya kweli na uzima,” alisema mama huyo.
GPL

No comments:
Post a Comment